Bunge la Israel wiki hii limeidhinisha hatua ya kwanza ya muswada unaopendekeza hukumu ya kifo kwa wapiganaji wa Palestina wanaohukumiwa kwa mauaji ya raia wa Israel.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya wabunge nchini Israel wanaamini kwamba hatua hiyo itazuia matukio ya kubadilishana wafungwa katika siku zijazo.

Wakati wa upigaji wa kura Jumatatu ya wiki katika hatua ya kwanza kati ya nne zinazohitajika kwa muswada huo kuwa sheria, wabunge 39 waliunga mkono wakati 16 wakiuupinga kati ya wabunge 120.

Waziri wa ulinzi wa kitaifa wa Israel, Itamar Ben-Gvir alikuwa ametoa wito kwa pande zote za kisiasa nchini humo kuunga mkono muswada huo ambao alisema unalenga kupambana na ugaidi.

“Hivi ndivyo namna tunapiga vita ugaidi, hivi ndivyo namna tunavyozuia, baada ya sheria hiyo kupitishwa, magaidi wataachiwa tu kwenda jehanamu.” Alisema Itamar Ben-Gvir.

Baada ya wabunge kuupitisha hatua ya kwanza ya muswada huo, Waziri wa ulinzi wa Israel Ben-Gvir aliwagawia peremende.

Kwa sasa muswada huo unasubiri kwenda katika hatua ya kamati ya bunge kwa mjadala zaidi kabla ya awamu ya pili na ya tatu ya upigaji kura.

Hadi sasa hakuna uhakika kwamba muswada huo utakuwa sheria baada ya vyama kadhaa vya kisiasa kususia kikao cha Jumatatu bungeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *