Makabiliano kati ya makundi mawili tofauti ya wanajihadi kaskazini mwa Nigeria yanaripotiwa kusababisha vifo vya takriban watu 200, katika eneo la ziwa Chad, kwa mujibu wa vyanzo vya kiintelejensia na wanajihadi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Makabiliano kati ya kundi la Boko Haram na wanajihadi kutoka kundi hasimu la ISWAP yalizuka katika eneo la Dogon Chiku, mwishoni mwa wiki iliopita.

Kulingana na vyanzo vya kijeshi, waliouawa katika vita hivyo ni wapiganaji wa kundi la ISWAP, taarifa ambayo pia ilithibitishwa na mwanajihadi wa zamani wa Boko Haram ambaye amekuwa akifuatilia shughuli za makundi hayo katika eneo hilo.

Aidha taarifa zingine zinasema kuwa kundi la Boko Haram kwa upande wake lilipoteza wapiganaji wake wanne, huku makabiliano hayo yakitajwa kuwa mabaya zaidi kushuhudiwa tangu pande hizo mbili zianze kushambuliana.

Kwa mujibu wa chanzo cha kijasusi nchini Nigeria kinachofanya kazi katika eneo hilo kinafuatilia matokeo ya mapigano hayo, huku kikikadiria kwamba waliouawa ni zaidi ya 150.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *