Umoja wa Mataifa, unataika dunia, kuingilia kati haraka mzozo wa Sudan, ili kukomesha mauaji na visa vingine vya kikatili vinavyoendelea katika nchi hiyo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Volker Turk, Mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za binadamu, ameliambia Shirika la Habari la AFP kuwa, mataifa ya dunia hapaswi kusubiri mauaji yanayoendelea nchini Sudan kutajwa kuwa ya kimbari kabla ya kupaza sauti.
Tangu kuanza kwa vita kati ya jeshi na wanagambo wa RSF mwezi Aprili mwaka 2023, mauaji makubwa yakiwemo ya kikabila yameendelea kuripotiwa nchini humo, huku mamilioni wakisalia wakimbizi.

Turk, amesema raia wa Sudan wanaishi katika mazingira magumu kwa sababu ya vita, ambapo wanakabiliwa na uhaba wa chakula na maji, huku kukiwa na ripoti kuwa baadhi yao sasa wanalazimika kula vyakula vya wanyama ili kuishi.
Mbali na mauaji, Mkuu huyo wa Tume ya Umoja wa Mataifa anasema kuna ripoti za ubakaji wa halaiki unaoendelea kwenye maeneo yenye vita, hasa katika mji wa El-Fasher.