Mahakama ya juu zaidi nchini Guinea imeuidhinisha kiongozi wa serikali ya kijeshi Mamady Doumbouya kuwania katika uchaguzi wa urais wa mwezi ujao.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kando na Doumbouya, wagombea wengine wanane wameidhinishwa kuwania kwenye uchaguzi huo unaolenga kurejesha utawala wa kiraia baada ya kufanyika kwa mapinduzi ya kijeshi nchini humo.
Doumbouya amekuwa akiongoza taifa hilo la Afrika Magharibi tangu kuchukua madaraka mwaka wa 2021 kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi.
Licha ya ahadi yake ya kurejesha utawala wa kiraia, alibadili nia na kuamua kuwania kwenye uchaguzi huo wa Disemba 28.

Siku ya Jumatano jioni wiki hii, mahakama ya juu ilichapisha majina ya mwisho ya wagombea tisa kati ya 51 ambao walikuwa wameonyesha nia ya kuwania kwenye uchaguzi huo.
Waziri Mkuu wa zamani ambaye ndiye kiongozi wa upinzani Cellou Dalein Diallo amezuiliwa kuwania kwenye uchaguzi.