
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio ametoa wito wa hatua za kimataifa kuchukuliwa ili kukomesha silaha zinazopokezwa kundi la RSF nchini Sudan, kufuatia ripoti za mauaji ya watu wengi katika eneo la El-Fasher.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Katika kilele cha mkutano wa G7 wa mawaziri wa mambo ya nje nchini Canada, Rubio amesema wapiganaji wa RSF walitekeleza ukatili, ikiwa ni pamoja na mauaji, ubakaji, unyanyasaji wa kingono dhidi ya raia, huku watoto na wanawake wakiathirika pakubwa.
Rubio, amesema RSF haina kiwanda cha kutengeza silaha na hivyo inategemea msaada kutoka nje, akitoa wito kwa nchi zinazowasambazia silaha kuacha.
Mwadiplomasia huyo amewaambia waandishi wa habari kuwa ili vita ya Sudan imalizike kunahitajika ushirikiano wa nchi mbalimbali wakati huu akipinga jaribio la RSF la kulaumu mauaji hayo kwa wahalifu.
Jeshi la Sudan, linaishtumu nchi ya Falme za Kiarabu kwa kuunga mkono kundi hilo kwa silaha na mamluki wanaotumwa kupitia nchi za Afrika, madai ambayo UAE mara kwa mara imekanusha.