Rais wa Marekani Donald Trump, ametia saini mswada unaositisha kukwama kwa shughuli za serikali, hali ambayo imekuwa ikishuhudiwa kwa siku 43.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja, baada ya bunge la wawakilishi kupitisha mswada huo muhimu, unaruhusu upatikanaji wa fedha wa kuendeleza shughuli za serikali na kuwalipa wafanyakazi, baada ya kukwama kwa kipindi kirefu katika historia ya nchi hiyo.

Rais Trump, amesema kutia saini kwa mswada huo, unatuma ujumbe kwa chama cha Democratic, anachosema kimejaribu kukwamisha ajenda yake kwa zaidi ya siku 40.

Katika siku hizo 43 za kukwama kwa shughuli za serikali, maelfu ya wafanyakazi wa serikali wamekwuwa wakifanya kazi, bila malipo, huku wengine wakiachishwa kazi kwa ukosefu wa fedha.

Chama cha Democratic kilikuwa kimekataa kuunga mkono kupitishwa kwa mswada muhimu wa upatikanaji wa fedha ili kuendesha serikali, ili kumshinikiza rais Trump kuachana na mpango wa kuondoa bima ya afya kwa wote, kabla ya baadhi ya wanachama hicho kubadilisha mawazo na kuunga mkono mwswada huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *