Sudan Kusini, Rais Salva Kiir amemfuta kazi Makamu wa kwanza wa Rais Benjamin Bol Mel, aliyekuwa akionekana kama mwanasiasa aliyekuwa anaandaliwa kumrithi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Tangazo la kufutwa kazi kwa makamu huyo wa rais kiir lilisomwa kupitia televisheni ya taifa bila kutolewa sababu rasmi, likiwa limeibua maswali kuhusu mwelekeo wa siasa za nchi hiyo.
Bol Mel ni mfanyabiashara mashuhuri na mfadhili wa serikali ambaye alipanda haraka katika ngazi za uongozi mwaka huu na alionekana kuwa mrithi wa Kiir, lakini sasa hatima yake ya kisiasa imegeuka ghafla baada ya kufutwa kazi.

Wachambuzi wanasema kuondolewa kwake kunaonesha migawanyiko ndani ya chama tawala, wakati huu ambapo makubaliano ya kugawana madaraka kati ya Kiir na mpinzani wake wa mda mrefu Riek Machar yakiendelea kuyumba.
Hata hivyo, licha ya umaarufu wa Benjamin Bol Mel, aliwekewa vikwazo na Marekani mwaka 2017 kwa tuhuma za ufisadi.