Mamlaka nchini Kenya imesema raia wake 200-wanapigana vita vya Ukraine kwa niaba ya Urusi, kukiwa na hofu kuwa huenda wengine wakasajiliwa kujiunga kwenye mzozo huo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Waziri wa mambo ya kigeni wa Kenya- Musalia Mudavadi, baadhi ya Wakenya wanaopigana kwa niaba ya Urusi ni wale waliowahi kuhudumu katika sekta ya usalama nchini Kenya.

Baadhi ya wale ambao tayari wameokolewa kutoka kwenye vikosi vinavyoiipigania Urusi wamesema walilazimishwa kutegeneza droni pamoja na kugusa kemikali bila ya kupewa mafunzo yanayohitajika wala kuvalia mavazi spesheli.

Rais wa Kenya William Ruto wiki iliopita alitoa wito kwa serikali ya Ukraine kusaidia kuachiwa kwa raia wa Kenya wanaoshikiliwa katika maeneo yenye mzozo.

Karibia raia 1,400 kutoka bara Afrika wanaisaidia Urusi katika vita vyake dhidi ya Ukraine, baadhi wakiwa wamesajiliwa kuwa wapiganaji baada ya kuhadaiwa, imesema serikali ya Ukraine.

Mwanariadha mchanga raia wa Kenya mwezi Septemba alikamatwa nchini Ukraine ambapo alisema kuwa alidaganywa kabla ya kujiunga na jeshi la Urusi.

“Zaidi ya Walenya 200 wamejiunga na jeshi la Urusi…. Mitandao ya usajili bado inaendelea nchini Kenya na Urusi,” alisema Musalia Mudavadi.

Mwezi Septemba, mamlaka nchini Kenya iliwaookoa raia wake 20 karibu na jiji kuu Nairobi ambao walikuwa wakijiandaa kujiunga katika vita vya Ukraine na Urusi

Afrika Kusini hivi karibu ilianzisha uchunguzi kuhusu namna raia wake 17 walifika katika Mji wa Donbas Mashariki mwa Ukraine kushiriki katika vita vinavyoendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *