Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Ijumaa ametangaza kuachana hadharani na mshirika wake wa muda mrefu na kiongozi wa MAGA Marjorie Taylor Greene Ijumaa, Novemba 14. Mbunge huyo wa Georgia alikuwa amekosoa waziwazi jinsi anavyoshughulikia suala la Epstein, kashfa ya kisiasa na kisheria ambayo imeikumba Ikulu ya Marekani.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hili limesababisha mshtuko mkubwa miongoni mwa wabunge wa mrengo wa kulia nchini Marekani. Donald Trump ameachana hadharani na mbunge wa Georgia Marjorie Taylor Greene. “Ninaondoa uungwaji mkono wangu kwa mbunge Marjorie Taylor Greene,” ameandika kwenye mtandao wake wa Truth Social, akiongeza: “Maggie ‘mgonjwa’ hafanyi chochote ila KULALAMIKA, KULALAMIKA, KULALAMIKA” kuhusu mwakilishi wa Georgia (kusini mashariki).

Huu ni mgawanyiko wa kwanza muhimu ndani ya kambi ya MAGA tangu mwanzo wa muhula wa pili wa Trump, ambao, tofauti na muhula wake wa kwanza, umekuwa na nidhamu kali sana karibu na rais wa Marekani.

MAGA imemkosoa sana Trump

Marjorie Taylor Greene amekosoa hadharani sera za kiuchumi za rais wa Marekani, akimshutumu kwa kutozingatia vya kutosha suala la nguvu ya ununuzi. Amelaani haswa jinsi alivyoshughulikia kesi nyeti sana ya Jeffrey Epstein, siku chache kabla ya kura katika Baraza la Wawakilishi iliyolenga kulazimisha utawala wa Trump kutoa faili zinazohusiana na mhalifu huyu wa kingono na kitabu chake cha anwani cha kuvutia.

“Donald Trump ananishambulia kwa nguvu ili kunifanya mfano na kuwatisha Warepublican wengine kabla ya kura ya wiki ijayo,” Marjorie Taylor Greene amejibu kwenye mtadao wa kijamii wa X. Ameona “inashangaza jinsi anavyopigania” kuzuia kuchapishwa.

Katika ujumbe wake kuhusu katika mtadao wake wa Truth Social, Donald Trump amesema nia yake ya kuidhinisha mgombea mwingine wa mrengo wa kulia ambaye angempinga Marjorie Taylor Greene katika kura ya awali. Tishio hili linakuja takriban mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wa katikati ya muhula, ambapo viti vyote katika Baraza la Wawakilishi, ikiwa ni pamoja na kile cha mwakilishi wa Georgia, vinatarajiwa kunyakuliwa.

Mvutano kufuatia vikwazo vya uchaguzi

Chama cha Republican kimepata hasara kubwa katika chaguzi za hivi karibuni za serikali za mitaa, na sauti ndani ya safu yake zimekitaka kizingatie zaidi gharama ya maisha, jambo ambalo ni wasiwasi mkubwa kwa kaya. Mbali na hayo, suala la Epstein linasababisha msukosuko mkubwa ndani ya kambi ya MAGA, ambayo inafuatilia kwa karibu hali hiyo. Donald Trump, ambaye mwenyewe alishirikiana na mfadhili huyo wa zamani, aliahidi ufunuo wakati wa kampeni yake lakini amekuwa akifanya kila awezalo tangu aliporejea Ikulu ya White House kufunga kesi hiyo.

Mnamo Novemba 14 rais wa Marekani alidai kwamba “hakujua chochote” kuhusu vitendo vya Jeffrey Epstein, ambaye alijiua gerezani kabla ya kesi yake ya biashara haramu ya ngono. Kesi hiyo ilizinduliwa wiki hii kwa kutolewa kwa barua pepe za Epstein, na vyombo vya habari vya Marekani vinaripoti kwamba Warepublican wengi watapiga kura wiki ijayo kuunga mkono kutolewa kwa hati za Wizara ya Sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *