
Tangu kuanza kwa vita nchini Sudan mnamo mwezi Aprili 2023, ripoti kadhaa za wataalamu wa Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa zimetaja kuwepo kwa usafirishaji haramu wa mafuta kati ya Libya pande wa Marshal Khalifa Haftar na Vikosi vya Msaadai wa Haraka (RSF) nchini Sudan.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Usafirishaji haramu huu umeongezeka, kulingana na ripoti mpya iliyochapishwa siku ya Alhamisi hii, Novemba 13, na Shirika lisilo la Kiserikali la Marekani The Sentry. Mbabe wa zamai wa kivita mashariki na kusini mwa Libya hutoa mafuta haramu kwa RSF badala ya “msaada muhimu” annaopokea kutoka Falme za Kiarabu kwa muongo mmoja uliopita.
Katika utafiti uliopewa jina la “Kambi ya Haftar ni muuzaji mkuu wa mafuta kwa RSF,” The Sentry inadai kwamba mafuta hayo, ambayo kimsingi yanatokana na usafirishaji haramu, yamewezesha “Vikosi vya RSF na shughuli za kimkakati huko Darfur, ambazo ziliangukia chini ya udhibiti kamili wa Vikosi vya Msaada wa Haraka mwishoni mwa mwezi Oktoba.”
Vifaa hivi vinaonyesha “uaminifu mkubwa wa familia ya Haftar kwa serikali ya Imarati,” ambayo ni “msaidizi mkubwa wa RSF,” ripoti inasema. Shirika hilo lisilo la kiserikali linaelezea kwamba lilitafuta maoni bila mafanikio kutoka UAE. Sentry inaendelea kusema kwamba “kutokana na usaidizi wa kiitikadi, kidiplomasia, kifedha, na kisiasa wa UAE kwa familia ya Haftar tangu mwaka 2014,” nchi hiyo “inachukua nafasi ya upendeleo machoni pa vikosi vya Haftar, na kuifanya iwe na deni kwa Abu Dhabi.”
Biashara inayoongezeka kwa kasi
Hata hivyo, ripoti inabainisha, utoaji wa mafuta na misaada mingine kwa RSF umeiwezesha familia ya Haftar kuimarisha “mamlaka yake na udhibiti wa kusini mashariki mwa Libya,” eneo linalopakana na Sudan.
Kukamatwa kwa pembetatu ya mpaka kati ya Libya, Sudan, na Misri mnamo mwezi Juni 2015 kuliongeza kwa kiasi kikubwa kasi ya biashara hii haramu. Hii imesababisha uhaba mkubwa wa mafuta kwa wakazi wa kusini mwa Libya, ambao hutumia saa nyingi wakisubiri katika vituo vya mafuta visivyo na kitu. Bei ya petroli inafadhiliwa na serikali ya Libya, nchi pekee duniani ambapo mafuta ni ya bei nafuu kuliko maji.
Ikumbukwe kwamba duru za kuaminika zimekuwa zikiripoti kiwango cha usafirishaji huu kwa miezi mingi. Picha za magari ya kijeshi yanayosafiri katika barabara ya jangwa kati ya kusini mwa Libya na Darfur zinaonyesha “madumu” yenye rangi la bluu zyaliyojaa mafuta, au tenki za mafuta ambazo wakati mwingine zimeshambuliwa na ndege za kijeshi za Sudan baada ya kuingia nchini Sudan.
“Kulinda na kuratibu” upitishaji wa rasilimali za kijeshi
Kulingana na shirika lisilo la kiserikali, vikosi vya Haftar vimeimarishwa kwa vifaa na wafanyakazi ili “kudumisha usafirishaji usiokatizwa wa mafuta na bidhaa zingine kuvuka mpaka” na kuhakikisha “udhibiti mkali wa mali muhimu” kama vile uwanja wa ndege wa Kufra au kiwanda cha kusafisha mafuta cha al-Sarir, ambacho “hufanya kazi karibu kwa ajili ya usafirishaji haramu kuelekea kusini,” ripoti hiyo inaongeza. Inasema zaidi kwamba vikosi vya Saddam Haftar “vinalinda na kuratibu” upitishaji wa rasilimali za kijeshi zinazotolewa kwa RSF huko Darfur na UAE kupitia Libya.