Nchini Senegal, kufuatia mzozo kati ya rais na waziri mkuu wake, upatanishi sasa ndio utaratibu wa kila siku ili kuepuka kuzorota kwa taasisi. Mzozo wa madaraka kati ya Ousmane Sonko na Bassirou Diomaye Faye kuhusu ni nani anayepaswa kuongoza muungano wa rais umegeuka kuwa mgogoro ndani ya wingi wa kambi ya rais, ambapo kila mtu anachagua upande wake.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Dakar, Léa-Lisa Westerhoff

Katika saa 48 zilizopita nchini Senegal, wapatanishi kadhaa wamekutana na viongozi wawili katika serikali. Viongozi wa kidini wa Mouride na familia za rais na waziri mkuu wake pia wameripotiwa kuhamasishwa, kulingana na vyanzo kadhaa. Miito ya utulivu imeongezeka kwenye mitandao ya kijamii. Hakuna matokeo halisi ambayo bado yametolewa hadharani. “Asili ya mvutano ni kwamba hatimaye zinapungua,” anasema muangalizi wa kisiasa anaye fahamu vema faili hiyo.

Wakati Waziri Mkuu akiendelea kutoa wito wa mageuzi ya mahakama ili kuifanya iwe huru zaidi, Bassirou Diomaye Faye alikutana na Rais wa Baraza la Katiba mnamo Novemba 14 kujadili “mageuzi yajayo ya kuimarisha utawala wa sheria,” kulingana na taarifa kutoka kwa ofisi ya rais.

Wakati huo huo, Wizara ya Fedha ilituma barua kwa wawekezaji. Barua hii ililenga kuwahakikishia dhamira ya Senegal ya kuendelea na majadiliano na Shirika la Fedha la Kimataifa na kuheshimu majukumu yake ya deni yanapostahili, kutokana na dalili za hivi karibuni za kutoaminiana katika masoko ya fedha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *