Baraza la Maaimamu nchii Tanzania limeelezea kusikitishwa na vifo vya kikatili vilivyotokea wakati wa uchaguzi nchini humo.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu jijini Dar es Salaam, Élodie Goulesque

Katika hotuba iliyotolewa siku ya Jumamosi, Novemba 15, Sheikh Issa Ponda “alilaani vikali” “mauaji ya watu wasio na hatia wakati wa uchaguzi.” Kauli hii inathibitisha zaidi ukubwa wa ukandamizaji ambao umelenga maandamano dhidi ya utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan kufuatia uchaguzi wa Oktoba 29.

Maneno hayo ni ya wazi na hayajasahaulika katika nchi ambapo dini ina jukumu muhimu katika maisha ya kila siku: “Tunalaani vikali mauaji ya watu wasio na hatia wakati wa uchaguzi,” Baraza la Maimamu wa Tanzania lilitangaza siku ya Jumamosi, Novemba 15. Katika taarifa, Sheikh Issa Ponda pia alitaja kwamba miongoni mwa waathiriwa wa vurugu zilizoiingiza nchi kwenye maombolezo kufuatia uchaguzi wa rais na wabunge wa Oktoba 29, baadhi ya watu waliuawa walipokuwa njiani kwenda kazini au walipokuwa nyumbani.

Ingawa taasisi hiyo ya kidini pia ililaani makosa mengi wakati wa uchaguzi na wakati wa zoezi la uhesabuji kura, zaidi ya vifo 1,000 kulingana na mashirika yasiyo ya kiserikali—taarifa hii kimsingi inathibitisha, tena, ukubwa wa ukandamizaji wa umwagaji damu wa maandamano ya baada ya uchaguzi dhidi ya utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan, ukandamizaji ambao tayari ulishutumiwa na wengine hapo awali.

Hotuba ya Sheikh Issa Ponda inaongeza orodha ndefu ya ukosoaji ulioelekezwa kwa serikali ya Tanzania tangu mwisho wa mwezi uliopita. Wiki iliyopita, maaskofu 41 walitaka uchunguzi huru—kwa ushiriki wa wachunguzi wa kimataifa—ili kutoa ukweli khusu “mauaji ya kikatili” yaliyofanyika baada ya  uchaguzi.

Familia nyingi zinaendelea kuzika au kutafuta ndugu zao waliofariki. Ingawa vyombo vya habari vya Tanzania viliepuka kwa uangalifu kutaja sehemu hii ya hotuba ya kiongozi wa kidini, badala yake wakizingatia mapendekezo yake ya maridhiano—neno ambalo Rais Samia Suluhu Hassan alirudia mara nyingi katika hotuba yake ya ufunguzi kwa Bunge siku ya Ijumaa, Novemba 14—utuklivu umerejea shughuli zinaendelea kama kawaida tu nchini kote Tanzania. Hata hivyo familia nyingi zinaendelea kuzika au kutafuta kimya kimya ndugu zao waliouawa, kama inavyothibitishwa na video ya kuhuzunisha iliyosambazwa sana kwenye Instagram. Katika hali ya vilio vya kushtua, mwanamume mmoja anaonekana akizika fulana, viatu vya michezo, na mali nyingine za kibinafsi katika shimo dogo lililochimbwa ardhini—mabaki yote ya kijana anayeitwa Kelvin, ambaye hajarudi nyumbani tangu Oktoba 29 na ambaye familia yake haijawahi kupata mwili wake.

Kutokana na hali hii, na licha ya rais aliyechaguliwa tena kwa 98% ya kura, kujariu kutuliza hisia—siku ya Ijumaa, alisema “amehuzunika sana” na vifo vya watu wengi katika ghasia za baada ya uchaguzi—wito wa maandamano mnamo Desemba 9 unaendelea kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *