Timu ya taifa ya DRC hapo jana iliweka hai matumaini yake ya kufuzu kucheza fainali za kombe la Dunia hapo mwakani baada ya kuwafungwa Nigeria kwa magoli 4 kwa 3 kwa njia ya Penaly baada dakika 90 miamba hiyo kutoka sare ya goli 1 kwa 1.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ushindi huu wa DRC unamaanisha kuwa imekata tiketi ya kuchezaja hatua ya mtoano ya mabara kwa ukanda wa Afrika huko Morocoo na sasa inasubiri kuchezeshwa kwa Droo mwezi Machi ambapo timu 6 zitachuana kutafuta washindi wawili watakaokamilisha timu 48.

Mechi za mtoano huko Rabati, Morocoo zilikuwa ni kwa timu zilizomaliza katika nafasi ya pili kwenye makundi 9 ya ukanda wa Afrika ambapo mechi za awali zilimalizika mwezi uliopita na kupata tiketi ya moja kwa moja.

Egypt, Senegal, Afrika Kusini, Ghana, Cape Verde, Morocco, Ivory Coast, Algeria and Tunisia zenyewe tayari zimeshafuzu kwa fainali za mwaka 2026 kutoka Afrika.

Chancel Mbemba - Mchezaji wa Leopard ya Congo.
Chancel Mbemba – Mchezaji wa Leopard ya Congo. REUTERS – ABDELMJID RIZKOU

Nchi ya Bolivia kutoka ukanda wa Amerika Kusini Pamoja na New Caledonia kutoka ukanda wa Oceania pia zimepata tiketi ya kufuzu katika michuano ya timu 6 hatua ya mtoano, ambapo kutajumuisha pia timu kutoka Falme za Kiarabu au Iraq, Amerika Kaskazini, Kati na Carribean ambapo timu mbili zitafuzu kucheza fainali za kombe la dunia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *