Wiki ya kwanza ya mkutano kuhusu tabianchi unaoendelea katika mji wa Amazonia nchini Brazil, Belem, ilishuhudia matukio tofauti, ikiwemo maadamano ya amani ya mashirika ya Mazingira, yaliojumuisha jamii za kiasili kutoka eneo la Amazonia.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
RFI Kiswahili ilizungumza na Omar El Mawi, mwanaharakati wa mazingira kutoka Kenya ambaye katika wiki ya kwanza anasema kuna mwanga kuhusu kufikiwa makubaliano muhimu ya njia za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
“Inaonekana kwa kiasi kikubwa kwamba kuna uwezekano mkubwa halijafanyika bado ila kuna uwezekano kwamba mataifa yatakubaliana.” Amesema Omar El Mawi, mwanaharakati wa mazingira kutoka Kenya.

Wiki ya pili na ya mwisho ya majadiliano hayo inang’oananga Jumatatu hii.
Omar El Mawi anaeleza zaidi kile ambacho kinatarajiwa.
“Tunatarajia kwa kifupi mambo matatu ikiwemo nchi kukubaliana kuondokea matumizi ya mafuta ya visukuku.” Aliongeza kusema Omar El Mawi.

Katika hatua nyingine, shirika la kimataifa linalohusika na uhamiaji, IOM limetoa wito kwa mataifa kuwapokea bila masharti, wahamiaji wanaotoka katika mataiafa ambayo yameathirika pakubwa na mabadiliko ya tabianchi.
Taarifa ya mwandishi wetu aliyeko Belem, Brazil, Minzilet Ijai, imesomwa na Emmanuel Makundi….