Waendesha mashtaka kwenye Mahakama ya Kimataifa ya ICC, wanataka kiongozi wa kundi la Janjaweed Ali Muhammad Ali Abd-Al-Rahman, maarufu kwa jina la Ali Kushayb, ambaye wapiganaji wake walisababisha mauaji makubwa kwenye jimbo la Darfur nchini Sudan, wanataka ahukumiwe maisha jela.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Waendesha mashtaka hao wakiongozwa na  Julian Nicholls  wameiambia Mahakama,  Al-Rahman mwenye umri wa miaka  76, wakati mmoja  alitumia shoka kuua watu wawili na kumtaja kama mhusika mkuu na hatari kufuatia misururu wa vitendo vya ukatili dhidi ya watu wasio na hatia , katika eneo la Darfur zaidi ya miaka 20 iliyopita.

Oktoba 7, alipatikana na hatia kwa  kutekeleza makosa 27 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, hatua ambayo imeonekana kuwa mafanikio ya kwanza ya mahakama ya mahakama hiyo yanayohusishwa na mzozo huo.

Ali Muhammad Ali Abd-Al-Rahman- Aliyekuwa mbabe wa kivita nchini Sudan wakati akiwa katika mahakama ya ICC.
Ali Muhammad Ali Abd-Al-Rahman- Aliyekuwa mbabe wa kivita nchini Sudan wakati akiwa katika mahakama ya ICC. REUTERS – Piroschka Van De Wouw

Nao Mawakili wa Al-Rahman wanaapinga mapendekezo hayo ya waendesha mashtaka  wakimtaja mshitakiwa kuwa asiye na hatia na wakaahidi kuwasilisha maoni yao juu ya hukumu yake baadaye wiki hii.

Mzozo wa Darfur ulizuka kwa mara ya kwanza mwaka 2003 wakati waasi wengi wasio Waarabu walipochukua silaha dhidi ya serikali ya Sudan, wakiishutumu serkali kutenga  eneo la magharibi mwa nchi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *