Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake Volodymyr Zelensky, wametia saini mkataba, ambao utaiwezesha Ukraine,kununua ndege za kivita 100 aina ya Rafale,  na vifaa vingine, ili kusaiadia katika vita dhidi ya Urusi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya rais nchini Ufaransa, imethibitisha hatua hii baada ya viongozi hao kukutana siku ya Jumatatu asubuhi, katika kambi ya jeshi ya Villacoublay, Kusini Magharibi mwa jiji la Paris.

Mbali na ndege hizo za kivita, Ukraine pia itapata mitambo ya kisasa aina ya SAMP-T yenye uwezo mkubwa wa kuzuia mashambulio ya angani.

Ziara ya Zelensky, nchini Ufaransa imekuja, baada ya ripoti za wanajeshi wa Urusi, kuripotiwa kusonga mbele kwa lengo la kudhibiti mji wa Pokrovsk.

Ufaransa imekuwa mshirika mkubwa wa Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi
Ufaransa imekuwa mshirika mkubwa wa Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi AFP – CHRISTOPHE ENA

Rais huyo wa Ukraine, kabla ya kukutana na Macron, alisema mkataba huo ni wa kihistoria huku, Ufaransa nayo ikisema, hatua hiyo itasaidia Ukraine kuendelea kupambana na uvamizi wa Urusi.

Mwezi uliopita, rais Zelensky pia aliingia kwenye makubaliano mengine ya kununua ndege za kivita kati ya 100 hadi 150 aina ya Gripen, kutoka kwa serikali ya Sweden.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *