
Moscow imedaileo Jumatatu, Novemba 17, kuteka vijiji vitatu vipya kwenye mstari wa mbele wa mashariki nchini Ukraine, ambapo jeshi la Urusi linaendelea kusonga mbele hatu kwa hatua dhidi ya vikosi vya Ukraine idadi yake imepungua.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema kwenye Telegram kwamba vikosi vya Urusi vimechukua udhibiti wa vijiji vya Platonivka katika jimbo la Donetsk, Dvoritchanské katika jimbo la Kharkiv, na Gaï katika jimbo la Dnipropetrovsk, kulingana na shirika la habari la AFP.
Siku ya Jeshi la Urusi lilidai kuwa liliteka vijiji viwili katika jimbo la Zaporizhzhia kusini mwa Ukraine, ambapo tayari lilikuwa limetangaza wiki hii kutekwa kwa maeneo mengine mawili.
Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilmeoa picha za angani za Rivnopillia, zikiwaonyesha wanajeshi wa Urusi wakipeperusha bendera za Urusi juu ya nyumba kadhaa zilizoharibiwa katika kijiji hicho, lakini AFP haikuweza kuthibitisha picha hizo.
Mnamo mwezi Septemba, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alionya kwamba Moscow ilikuwa ikikusanya wanajeshi katika sehemu iliyokaliwa ya jimbo la Zaporizhzhia katika maandalizi ya mashambulizi.
Mbali na mapigano katika mstari wa mbele, Urusi inaendelea kushambulia miundombinu ya nishati kote Ukraine kwa makombora na ndege zisizo na rubani.