Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky leo Jumatatu, Novemba 17, amepokelewa mjini Paris na mwenyejiwake, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. Ziara hii, ya tisa ya Rais Zelensky nchini Ufaransa tangu kuanza kwa vita nchini Ukraine, inakusudiwa, kulingana na Ikulu ya Élysée, kuthibitisha tena kujitolea kwa Ufaransa kwa Kyiv na “kudumisha kasi ya kazi inayofanywa katika suala la dhamana ya usalama ndani ya mfumo wa ‘muungano wa walio tayari’.”

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Baada ya Athens siku ya Jumapili, Paris ni kituo kinachofuata katika ziara ya rais Volodymyr Zelensky barani Ulaya. Pia anatarajiwa nchini Uhispania siku ya Jumanne, Novemba 18. Kiongozi huyo wa Ukraine anatarajiwa kuwahakikishia wenzake wa Ulaya baada ya kashfa inayohusisha ubadhirifu wa dola milioni 100 na baadhi ya washirika wake wa karibu katika sekta ya nishati.

Katika mahojiano na Gazeti la Politico kuhusu kashfa hii ya ufisadi, chanzo kilicho karibu naIkulu ya Élysée kimesema kwamba uhusiano kati ya Paris na Kyiv unategemea “uaminifu na heshima” na kwamba Waukraine “wanajua kile Ufaransa inatarajia kutoka kwao.”

“Makubaliano makubwa yanaandaliwa”

Zelensky na Macron wanatarajiwa kujadili mahitaji ya kijeshi ya Kyiv na ushirikiano kati ya viwanda vya ulinzi vya nchi hizo mbili, huku kiongozi wa Ukraine akirejelea “makubaliano makubwa yanaandaliwa.” Kulingana na Ikulu ya Élysée, lengo ni “kuweka ubora wa Ufaransa katika tasnia ya silaha katika huduma ya ulinzi wa Ukraine” na “kuwezesha upatikanaji wa mifumo muhimu ili kukabiliana na uchokozi wa Urusi.”

Ofisii ya rais wa Ufaransa imetaja haswa “ulinzi wa anga ya Ukraine,” huku Volodymyr Zelensky akirudia wito wake Jumamosi kwa mifumo zaidi ya ulinzi wa anga, siku moja baada ya mashambulizi mapya makubwa ya anga ya Urusi dhidi ya nchi yake.

Rais wa Ufaransa na mwenzake wameanza siku yao katika kambi ya kijeshi ya Villacoublay. Rais wa Ukraine, ambaye mwezi uliopita alisaini barua ya nia ya kupata ndege za kivita za Gripen 100 hadi 150 kutoka Sweden , ataonyeshwa ndege ya kivita ya Ufaransa ya Rafale na silaha zake, pamoja na mifumo ya ndege zisizo na rubani na mfumo wa ulinzi wa anga wa kizazi kijacho wa SAMP-T. Ndege ya mwisho imepangwa kupelekwa Ufaransa kuanzia mwaka wa 2027 na imeongeza uwezo wa kuzuia makombora ikilinganishwa na SAMP-T, ambayo moja tayari imetumwa Ukraine.

Mifumo ya ulinzi wa anga

“Tunafanya kazi katika utoaji wa mifumo kadhaa ya ulinzi wa anga na kuimarisha jeshi letu la anga,” Volodymyr Zelensky alitangaza katika video siku ya Ijumaa, akiongeza kuwa “makubaliano makubwa yanaandaliwa na Ufaransa.” “Yatakamilishwa haraka sana, nina uhakika nayo; yatakuwa ya kihistoria,” aliongeza.

Emmanuel Macron na Volodymyr Zelensky pia wamepangwa kutembelea makao makuu ya “kikosi cha kimataifa cha Ukraine,” ambacho Ufaransa na Uingereza zinafanya kazi kukianzisha. Kikosi hiki kitatumwa kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano na “dhamana za usalama” zinazotolewa kwa Kyiv.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *