Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, hapo jana alitangaza baraza lake la mawaziri 27, akiwaacha nje mawaziri 7 waliohudumu katika serikali iliyopita.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Miongoni mwa walioachwa ni pamoja na aliyekuwa naibu Waziri mkuu na Waziri wa nishati, Dotto Biteko, Waziri wa kilimo Hussein Bashe, Waziri wa mambo ya ndani Innocent Bashungwa na aliyekuwa Waziri afya Jenista Muhagama.
Wengine ni aliyekuwa Waziri wa sheria, viwanda na biashara Pamoja na wizara ya afya.
Walioteuliwa ni Pamoja na Waziri wa fedha, Khamis Mussa Omar, huku akimuacha Waziri wa mambo ya nje Thabit Kombo.

Baadhi ya Mawaziri wapya ni Pamoja na Joel Nanauka aliyeteuliwa kuwa Waziri wa vijana, Paul Makonda aliyeteuliwa kuwa naibu Waziri wa sana ana utamaduni na Daniel Chongolo aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo.
Kwenye uteuzi huo pia alimpandisha cheo mtoto wa rais wa zamani Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete kuwa Waziri wa utumishi wa umma na utawala bora, huku mwanawe wa kike Wanu Hafidh Amir akiteuliwa kuwa naibu Waziri wa elimu.
Juma lililopita alimteua aliyekuwa waziri wake wa fedha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri mkuu.
Uteuzi wa baraza lake la mawaziri umekua siku chacje tangu achaguliwe kuwa rais kwa kupata ushindi wa asilimia zaidi ya 97, uchaguzi ambao uligubikwa na vurugu, huku upinzani ukipinga ushindi wake na kukashifu vifo vya raia.