Italia italazimika kushinda mechi mbili za mchujo mwezi Machi mwakani ili ikate tiketi ya kushiriki Fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakazofanyika Canada, Mexico na Marekani.

Baada ya kushindwa kufuzu moja kwa moja kufuatia kumaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi I, Italia sasa imebakiza matumaini ya kucheza fainali hizo kupitia mechi hizo mbili za mchujo inayohusisha timu za bara la Ulaya tu.

Katika mechi hizo za mchujo, Italia imepangwa kukutana na Ireland Kaskazini ambapo ikishinda itaumana na mshindi baina ya Wales na Bosnia&Herzegovina kusaka tiketi moja ya kwenda Kombe la Dunia.

Ikumbukwe Italia haijafuzu Fainali za Kombe la Dunia mara mbili mfululizo zilizopita zilipofanyika Qatar na Russia.

Katika droo ya mechi hizo za mchujo iliyofanyika leo huko Ukraine imepangwa kucheza na Sweden na mshindi atakutana na timu itakayoshinda baina ya Poland na Albania.

Uturuki itakutana na Romania na mshindi atakutana na kinara wa mechi kati ya Slovakia na Kosovo.

Nayo Denmark imepangwa kucheza na Macedonia Kaskazini na timu itakayoshinda itakutana na ama Jamhuri ya Czech au Jamhuri ya Ireland.

DR Congo kukutana na huyu

Droo hiyo ya leo pia imegusa na mechi za hatua ya mwisho ya mchujo ya mabara tofauti na Ulaya kusaka tiketi mbili za Kombe la Dunia.

Wawakilishi wa Afrika, DR Congo wao watakutana na mshindi baina ya New Caledonia na Jamaica na mshindi atafuzu Kombe la Dunia.

Bolivia itakutana na Suriname na mshindi atawania tiketi moja dhidi ya Iraq.

Mechi za kwanza zitachezwa Machi 26 mwakani na za mwisho zitachezwa Machi 31, 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *