Polisi nchini Tanzania, wanaoshtumiwa na wapinzani na waharakati wa kutetea haki za binadamu kwa kutekeleza mauaji ya mamia ya watu wakati wa uchaguzi mkuu mwezi uliopita, wameonya kuhusu mpango wa kufanyika kwa maandamano tarehe 9 mwezi Desemba.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Jeshi la polisi nchini humo limeonya kuhusu mpango wowote wa kuandaa maandamano hayo, na kuonya kuwachukulia hatua wale wanaopanga maandamano hayo.
Aidha, polisi wameonya kuwa, machafuko yoyote, yataleta madhara ya kiuchumi, kijamii na kiusalama kwa Watanzania wote.

Onyo hili la polisi limekuja, huku wanaharakati wakiitisha maandamano ya amani Desemba tarehe 9 siku ya uhuru wa Tanzania, baada ya machafuko yaliyotokea, kipindi cha uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwezi Oktoba.
Wiki hii rais Samia Suluhu Hassan, alitangaza tume ya ndani kuchunguza kilichotokea, licha ya chama kikuu cha upinzani CHADEMA na ACT Wazalendo kusema haina imani na Tume hiyo.