Dar es Salaam. Je, video vixen ni nani hasa? Huyu ni mwanamke mwenye mvuto ambaye huonekana katika video za muziki hasa miondoko ya Hip Hop, R&B, Afrobeats, Bongofleva na aina nyingine za muziki.
Mara nyingi huyu ni mrembo anayejua kuonyesha mitindo ya uchezaji au uigizaji katika video kulingana na hadithi ya wimbo husika kwa lengo la kuipendezesha.
Neno ‘video vixen’ lilianza kushika kasi mapema miaka ya 2000 katika muziki huko Marekani kwa sabau video zilikuwa na matumizi makubwa ya wanawake warembo waliokuwa wakicheza au kuigiza.
Baadhi ya mastaa kama Nelly, Usher, Ludacris, Jay Z, 50 Cent na Diddy, video za ngoma zao zilipendezeshwa na wanawamke wenye mvuto ambao ndio hao video vixens.
Mtindo huo kwa Bongo pia upo na kwa miaka ya hivi karibuni umetengeneza majina makubwa upande huo kama Hamisa Mobetto, Gigy Money na Amber Lulu ambao wametokea kwenye video za wasanii wengi.
Ila baadhi ya video vixens waliamua kuingia rasmi katika muziki wa Bongo Fleva wakirekodi nyimbo zao lakini kwa sasa maji yanaonekana kuwa marefu kwao kutokana na kukosa mwendelezo kama ifuatavyo.
Alitokea katika video nyingi, baadhi ya hizo ni Mazoea (2017) yake Billnass akimshirikisha Mwana FA na Usimsahau Mchizi (2017) ya kwao Roma na Centrozone ambaye aliwahi kuwa mpenzi wake.
Umaarufu wake ulikuja baada ya kuonekana katika video ya Darassa, Muziki (2016) aliomshirikisha Ben Pol, ni video ambayo sasa inashikilia rekodi Bongo kwa kutazamwa zaidi YouTube upande wa Hip Hop.
Nai alijitosa katika muziki akiwa chini ya lebo ya Akida OG Entertainment iliyokuwa inawasimamia wasanii wengine wakati huo kama Stamina, Rhino (wa kundi la The Mafik) na mchekeshaji Mkali Wenu.
“Mimi nimeingia kwenye kuimba kwa kupenda mwenyewe, siyo kwa sababu nimelazimishwa au kumuiga mtu yeyote. Navutiwa na Nandy anaimba vizuri, pia Zuchu yupo vizuri,” alisena Nai wakati huo.
Wimbo wake wa kwanza, Sio Saiz Yao (2021) alimshirikisha Sanja Kong, kisha akafanya kolabo nyingine na Baddest 47, Makubwa (2021) na baada ya hapo akaachana na kuimba moja kwa moja hadi hii leo.
Kazi ya kwanza kumleta katika macho ya umma ni video ya Rayvanny, Kwetu (2016), wimbo uliokuwa wa kwanza pia kwa mwanamuziki huyo chini ya WCB Wasafi na ndiyo uliomtambulisha katika tasnia.
Alifunika zaidi na kuzungumziwa alipotokea katika video ya Mbosso, Hodari (2018) akionyesha uwezo mkubwa kucheza. Ni kipindi alichokuwa akihusishwa kuwa na uhusiano na Diamond Platnumz, tetesi zilizokosa uthibitisho.
Baadaye Lyyn akaamua kuimba akitoa wimbo wake wa kwanza, Chafu (2018) ambao ulipata mapokezi mazuri kwa kiasi chake lakini hakuwa na mwendelezo mzuri, tunaweza kusema jedwali lake lilienda likishuka chini.
Ndani ya miaka hii sita ametoa nyimbo takribani 10 lakini kwa kunyata. Wimbo wa mwisho kuachia (Ntabaki Nawe) ulitoka mwaka mmoja uliopita huku idadi ya waliousikiliza katika mtandao ikiwa siyo ya kuridhisha.
Mathalani, licha ya Lyyn kuwa na wafuasi zaidi ya milioni 1.6 katika ukurasa wake wa Instagram, video ya ngoma yake, Mteke (2023), imetazamwa chini ya mara 5,000 YouTube ikiwa ni miaka miwili tangu itoke!.
3. Hamisa Mobetto
Ni takribani miaka mitatu sasa Hamisa Mobetto hajatoa wimbo wowote kwa mashabiki wake, pengine hii ni ishara kuwa ameamua kujipa likizo ndefu au ameachana na muziki moja kwa moja!.
Kazi ya mwisho kutoa ni video yake ‘Murua’ iliyotoka Desemba 2, 2022, wimbo huo ulikuwepo katika Extended Playlist (EP) yake ya kwanza, Yours Truly (2022) iliyotoka chini ya Mobetto Music.
Ikumbukwe Hamisa kabla ya kuingia kwenye uimbaji akiachia ngoma yake, Madam Hero (2018), alijulikana katika mambo mengi ya sanaa, na kati ya hayo ni kufanya kazi ya video vixen.
Video alizotokea Hamisa ni za Abdukiba, H Hatuna Habari Nao (2012), Barnaba, Magubegube (2012), Diamond, Mawazo (2012), Quick Rocka, My Baby (2013), Diamond, Salome (2016) na Alikiba, Dodo (2020).
Hamisa, mshindi wa pili Miss Dar Indian Ocean 2011, aliwahi kudai tangu akiwa mdogo alipenda sana kuja kuwa mwanamuziki ila kutokana na kutafuta fedha akajikuta ameingia kwenye filamu na mitindo kabla ya muziki.