Muungano wa Wakristo nchini Nigeria unasema wanafunzi na Walimu 315 walitekwa katika shambulio la watu wenye silaha Ijumaa ya wiki hii.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Shambulio la mapema Ijumaa dhidi ya shule St Mary’s school inayomilikiwa na kanisa Katoliki katikati mwa jimbo la Niger lilijiri baada ya lengine la Jumatatu ya juma hili katika shule jirani kwenye jimbo la Kebbi ambapo wasichana 25 walitekwa.
Kulingana na taarifa ya muungano huo, wanafunzi 303 na Walimu wao 12 walichukuliwa na watu wenye silaha katika shambulio hilo la Ijumaa.
Idadi ya wanafunzi waliotekwa inakaribia nusu ya wanafunzi wote kwenye shule hiyo yenye wanafunzi 629.

Kutokana na matukio haya ya utekaji nyara na mashambulio dhidi ya shule, mamlaka katika majimbo jirani ya Kastina na Plateau imeaagiza kufungwa kwa shule zote kama tahahdari kuzuia utekaji.
Serikali ya jimbo la Niger ilifunga sehemu kubwa ya shule kutokana na kuongezeka kwa visa vya utekaji, Rais Bola Tinubu alisitisha safari zake za kimataifa ikiwemo mkutano wa G20 nchini Afrika Kusini.
Tinubu alihairisha safari hizo kushugulikia changamoto za usalama kwenye taifa lake haswa wakati huu shinikizo zikiendelea dhid ya serikali yake kutatua suala hili.

Matukio la utekaji wa wanafunzi shule ikiwemo shambulio dhidi ya kanisa Magharibi mwa Nigeria yameongezeka tangu Rais wa Marekani Donald Trump kutishia kuchukua hatua za kijeshi kukabiliana na kile alichokiita kama mauaji ya Wakristo nchini Nigeria yanayotekelezwa na wapiganaji wa kiisilamu wenye itikadi kali.
Muongo mmoja uliopita karibia wanafunzi 300 wa kike walitekwa na wapiganaji wa Boko Haram katika Mji wa Chibok kaskazini mashariki mwa jimbo la Borno.Baadhi ya wasichana hao hawajapatikana hadi sasa.