India. Nyota mkongwe wa filamu za Kihindi, Dharmendra afariki dunia asubuhi ya leo Jumatatu akiwa na umri wa miaka 89 ikiwa ni siku chache tangu aliporuhusiwa kutoka hospitalini.

Taarifa kutoka Mumbai, India, zinasema kuwa mwingizaji huyo aliyetamba na filamu za Kidosi kwa miongo kadhaa sasa amekumbwa na mauti akiwa nyumbani kwake, siku chache tangu alipotolewa katika hospitali ya Breach Candy, Kusini mwa Mumbai.

Mwigizaji huyo aliyefahamika kwa kazi zilizomtambulisha kwa mashabiki wa filamu duniani kama kama Ayee Milan Ki Bela, Phool Aur Patthar, Aaye Din Bahar Ke, Seeta Aur Geeta, Raja Jani, Jugnu, Yaadon Ki Baaraat, Dost, Sholay, Pratiggya, Charas, Dharam Veer awali alilazwa hospitalini hapo na kuilazimisha familia yake kukanusha taarifa kwamba alikuwa mahututi.

DHAR 01

Mkongwe huyo amekumbwa na mauti wakati filamu mpya ya Ikkis aliyoishiriki ikitarajiwa kuachiwa rasmi Desemba 25, ikiwa ni siku ya Krismasi.

Kwa wanaomkumbuka vyema muigizaji huyo mwaka 1987 aliwasapraizi mashabiki kwa kuachia filamu saba ndani ya mwaka mmoja na zote zilibamba kwa ukali wake.

Filamu hizo ni Insaniyat Ke Dushman, Loha, Hukumat, Aag Hi Aag, Watan Ke Rukhwale, Mard Ki Zubaan na Dadagiri.

DHAR 02

Novemba 12 mwigizaji huyo aliruhusu kutoka hospitali ya Breach Candy, siku chache baada ya mwanae, Sunny Deol kukanusha taarifa zilizozagaa kwamba baba yake alikuwa ICU, lichja ya kukiri ni kweli alikuwa chini ya uangalizi kabla ya leo kukumbwa na mauti.

Mwaka 2023, aliigiza katika filamu Rocky Aur Rani Kii Prem Kahaani, iliyoongozwa na Karan Johar.

DHAR 03

Mkongwe huyo aliyezaliwa Desemba 8, 1935 na alianza kuigiza tangu miaka ya 1960 na kucheza zaidi ya filamu 100 kabla ya mwaka 2004 kugeukia siasa na katika umri wake amebahatika kupata watoto sita akiwamo Sunny Deol, Boby Deol n Esh Deol ambao nao ni waigizaji wa filamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *