#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Jabiri Makame, amefanya oparesheni ya kushtukiza kukamata wafanyabiashara wa mbolea Wilaya ya Mbozi ambao wamekuwa wakiuza mbolea ya Ruzuku kinyume na bei elekezi ya Serikali.
Oparesheni hiyo imefanyika kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa kwake na wakulima katika Jukwaa la Wadau wa Kilimo Mkoa wa Songwe kujadili mikakati ya kuendeleza Sekta ya Kilimo mkoani humo.
Akizungumza katika Oparesheni hiyo, RC Makame ametoa onyo kwa wafanyabiashara wote wa mbolea Mkoa wa Songwe kutojihusisha na uuzaji mbolea ya ruzuku nje ya mfumo, kuuza zaidi ya bei elekezi na kutothubutu kutorosha mbolea kwenda nje ya nchi kwani kufanya hivyo ni kudidimiza jitihada za Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kuwakomboa wakulima katika Mkoa wa Songwe.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania