Stéphane Dujarric, Msemaji wa Katibu Mkuu, amewaambia waandishi kwamba kiongozi huyo wa Umoja wa Mataifa anatoa wito kwa wadau wote wa kitaifa nchini Guinea-Bissau kuwa watulivu na kuzingatia utawala wa sheria wakati mivutano ikiendelea nchini humo.

Dujarric ameongeza kuwa Katibu Mkuu “ataendelea kufuatilia kwa karibu matukio yanavyojiri”, akisisitiza dhamira ya Umoja wa Mataifa katika kulinda uthabiti na kuhimiza mazungumzo ya amani katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Vyombo vya habari mbalimbali vya kimataifa ndani na nje ya Afrika vinaripoti kwamba baadhi ya maafisa wa jeshi wametwaa Madaraka ya nchi baada ya kutokea mvutano wa uchaguzi ambapo chama cha upinzani kimedai kunyang’anywa ushindi wake na Rais aliyekuwa mamlakani akiwania kurejea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *