Jeshi la Israel limetangaza leo Jumatano, Novemba 26, uzinduzi wa “operesheni kubwa” dhidi ya makundi yenye silaha ya Palestina kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi unaokaliwa.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Wakati wa usiku (Jumanne kuamkia Jumatano), vikosi (vya Israel) vilianza kufanya kazi kama sehemu ya operesheni kubwa ya kupambana na ugaidi katika eneo la kaskazini mwa Samaria,” jeshi limesema katika taarifa, likitumia jina la kibiblia ambalo Waisrael hutumia kurejelea kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi.

Jeshi la Israel ambali limehojiwa na shirika la habari la AFP, limebainisha kwamba hii haikuwa operesheni kama sehemu ya “operesheni yake ya kupambana na ugaidi” iliyozinduliwa mwezi Januari 2025, ambayo kimsingi inalenga kambi za wakimbizi wa Palestina katika eneo hilo, bali ni “operesheni mpya.” Jeshi la Israel halikutoa maelezo zaidi.

Vurugu zimezuka

Vurugu zimeongezeka katika Ukingo wa Magharibi tangu kuanza kwa vita vya Gaza, vilivyosababishwa na shambulio la umwagaji damu kusini mwa Israel na kudi la wanamgambo la Hamas mnamo Oktoba 7, 2023.

Tangu Oktoba 7, zaidi ya Wapalestina elfu moja, wakiwemo wapiganaji wengi lakini pia raia wengi, wameuawa katika eneo hilo na wanajeshi wa Israel au walowezi, kulingana na hesabu ya shirika la habari la AFP ikijikita kwenye data kutoka Mamlaka ya Palestina.

Wakati huo huo, kulingana na takwimu rasmi za Israel, angalau Waisrael 43, wakiwemo raia na wanajeshi, wameuawa katika mashambulizi ya Palestina au wakati wa mashambulizi ya kijeshi ya Israel. Vurugu zimeendelea bila kuzuiliwa katika Ukingo wa Magharibi tangu makualiano ya usitihaji mapigano huko Gaza yaliyoanza kutumika mnamo Oktoba 10.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *