
Katika taarifa yao ya mwisho iliyochapishwa siku ya Jumanne, Novemba 25, taasisi hizo mbili zimesifu ushirikiano wao “wa kipekee na wa kimkakati” na kutoa ahadi nyingi. Miongoni mwa ahadi hio ni pamoja ni pamoja na kuunga mkono na kukuza ushirikiano wa pande nyingi, kuimarisha uhusiano wao wa kibiashara, kukuza ushirikiano wao kuhusu madini ya kimkakati, na kupunguza uhamiaji haramu na kuwezesha uhamaji wa raia wa kambi zote mbili.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu maalum mjini Luanda, Paulina Zidi
Baada ya siku mbili za majadiliano na mikutano, wajumbe 80 walioalikwa Angola kwa mkutano wa saba wa Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Ulaya (EU) waliondoka katika mji wa Angola, Luanda, siku ya Jumanne, Novemba 25. Ingawa taarifa ya mwisho iliyotolewa na taasisi hizo mbili, ambazo zilisherehekea miaka 25 ya ushirikiano wao “wa kipekee na wa kimkakati” katika tukio hili, haikuwa na matangazo makubwa, ilijumuisha ahadi nyingi. Miongoni mwa ahadi hieo, haswa, ni kujitolea kuunga mkono na kukuza ushirikiano wa pande nyingi, suluhisho pekee la kuepuka “machafuko,” kulingana na Rais wa Baraza la Ulaya António Costa.
“Tunaporuhusu taifa lolote kukiuka amani na mipaka inayotambuliwa kimataifa ya nchi nyingine, tunawaruhusu wote kufanya vivyo hivyo. Ndiyo maana hakuna njia mbadala ya utaratibu wa pande nyingi na kimataifa unaotegemea sheria,” ametangaza, akisisitiza kwamba ushirikiano wa AU-EU umejengwa juu ya “maadili ya pamoja.”
“Tunahitaji kuweza kuuza nje kobalti, lakini pia betri za magari”
Kambi hizo mbili pia zilionyesha nia yao ya kuimarisha uhusiano wao wa kibiashara na kukuza ushirikiano wao katika madini ya kimkakati, jambo ambalo Afrika iliomba Ulaya hasa kuunda mambo yenye thamani. “Tunahitaji kuweza kuuza nje kobalti, lakini pia betri za magari,” alisema Tete Antonio, Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola na mwenyeji wa mkutano huo, ambapo changamoto nyingi zimesalia kwa nchi hiyo. “Tulijadili amani, usalama, na utawala, lakini zaidi ya yote, tulisisitiza kwamba lazima tufanye kazi ili kuhakikisha ustawi wa pamoja na kwamba maadili ya mshikamano, ushirikiano, na mazungumzo yanahifadhiwa,” aliongeza.
Ingawa uhamiaji pia ulikuwa mada kuu ya majadiliano, kwa lengo la kupunguza uhamiaji haramu huku ukikuza uhamaji wa raia, migogoro inayokabili mabara yote mawili pia ilikuwa muhimu kwa majadiliano: vita nchini Ukraine, bila shaka, lakini pia migogoro nchini Sudan na mashariki mwa DRC. Kuhusu Sudan na DRC, washiriki wa mkutano huo walilaani ukatili unaofanywa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) – haswa katika mji wa El-Fasher – na wakathibitisha tena uungaji mkono wao kwa Azimio la Umoja wa Mataifa 2773 na majadiliano huko Washington na Doha yaliyolenga kurejesha amani mashariki mwa Kongo, ambapo Ulaya haijachukua jukumu lake kikamilifu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji alikosoa.
“Umoja wa Ulaya unaweza kuwa ulikuwa mwepesi sana kuridhika na kuweka vikwazo mwezi Februari au Machi mwaka huu, bila kuzingatia maendeleo ya hali yenyewe.” “Na leo, sina uhakika kama vikwazo vipya vinafaa, kwa hatari ya kutumika kuhalalisha kuvuruga michakato inayoendelea ya upatanishi: ingawa lazima tuwe macho kuhusu dharura ya kibinadamu, hatupaswi kuruhusu simulizi zisizofaa kuelekeza kidole kwa EU kama ile ambayo hatimaye ilizuia makubaliano kufikiwa,” Maxime Prévost alitangaza.