Kremlin imeripoti leo Jumatano “mambo chanya” katika mpango wa Marekani wa kutatua mgogoro nchini Ukraine, huku ikisisitiza kwamba bado haijaijadili “kwa undani na mtu yeyote.”

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Baadhi ya mambo, tunaweza kusema, ni chanya, lakini mengine mengi yanahitaji majadiliano maalum miongoni mwa wataalamu,” mshauri wa masuala ya kidiplomasia wa Kremlin Yuri Ushakov ameiambia televisheni ya serikali ya Urusi.

Wakati huo huo Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz amesema leo Jumatano kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin lazima akubali kwamba hana nafasi ya kuibuka mshindi katika vita vya Ukraine, kulingana na shirika la habari la Reuters.

Merz ameongeza kuwa Ujerumani itaendelea kuwaunga mkono raia wa Ukraine na kwa lengo hili itatumia mali za Urusi zilizozuiliwa.

“Mustakabali wa Ukraine uko katika Umoja wa Ulaya,” anasema Ursula von der Leyen

Wakati wa hotuba yake kwa Bunge la Ulaya, Ursula von der Leyen amesema kwamba “mustakabali wa Ukraine uko katika Umoja wa Ulaya.”

Amebainisha kwamba makubaliano yoyote ya amani “lazima yahakikishe usalama wa kweli kwa Ukraine na Ulaya.”

Rais wa Tume pia amebaiisha kwamba “anakaribisha juhudi zinazoongozwa na Rais Donald Trump kwa ajili ya amani nchini Ukraine,” huku akionya dhidi ya makubaliano yoyote ambayo yatadhoofisha mipaka:

“Ikiwa leo tutahalalisha na kukubali kuhojiwa kwa mipaka, tunafungua mlango wa vita zaidi kesho, na hatuwezi kuruhusu hilo kutokea.”

Hatimaye, Ursula von der Leyen amebaini kwamba Tume ya Ulaya iko tayari kuwasilisha maandishi ya kisheria kuhusu matumizi ya mali za Urusi zilizozuiwa katika muktadha wa vita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *