Katika vijiji vya wafugaji, kila mnyama ana thamani sawa na maisha. Lakini miaka ya hivi karibuni vimekuwa na misimu isiyotabirika, ukame unaodumu miezi mingi, ukifuatiwa na mafuriko ya ghafla. Ndipo mradi wa bima ya mifugo na huduma za mifugo ukaanzishwa, ukiwafikia maelfu ya wafugaji. Mmoja wa walionufaika ni Amina Mohammed, mama wa watoto wanne kutoka kijiji cha Korakora.

Watoto wangu sasa wanasoma shule vizuri. Hapo awali walikuwa wakizurura barabarani, wakifuga tu. Lakini sasa wana sare za shule na wanahudhuria masomo kila siku. Mimi mwenyewe nimeongeza hata mbuzi wengine. Hii bima si pesa tu, ni elimu, ni kinga, na ni matumaini.”

Zaidi ya mawakala 60 wa vijiji vya eneo hilo wamefundishwa kuwasajiliwafugaji katika bima ya mifugo katika kaunti za Garissa na Isiolo. Bi Amina akiwa katika kikundi kinachoongozwa na mmoja wa Mawakala hao anasema , Akitaja shilingi 24,600 za Kenya ni sawa na dola US$190

Mimi ni mkazi wa Korakora, mama wa watoto wanne. Huyu ndiye wakala wa kijiji aliyekuja kutufundisha na kutueleza zaidi kuhusu mradi huu. Alituambia kwamba serikali inalipia asilimia 80 na sisi kama wafugaji tunachangia kiasi kidogo tu. Pia ametupa mifano ya watu ambao tayari wamenufaika, na kina mama tukashawishika haraka tukaanza kulipa. Maisha yakaendelea vizuri. Lakini kiangazi kilipokuja, Wanyama, hasa ng’ombe wakaanza kufa, na mbuzi wakadhoofika. Wasiwasi ukanijaa. Tulipozungumza na majirani, nao wakasema wameshapoteza mifugo yao. Nilipofika nyumbani, nilipokea ujumbe kwa simu kwamba nimepokea shilingi elfu ishirini na nne mia sita (24,600) ambayo ni sawa na dola $190.”

Mbali na bima, zaidi ya vikundi 200 vya akiba na mikopo ya kijamii vimeanzishwa ili kuwafundisha wafugaji kuweka akiba, kuelewa bima na kujenga mnepo wa kifedha. Hii inarahisisha upatikanaji wa elimu ya fedha kwa jamii ambazo hapo awali hazikuwa na fursa hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *