Licha ya juhudi za mashirika yasiyo ya kiserikali na mamlaka za afya, surua inaendelea kuathiri maeneo ya Masisi na Rutshuru  katika mkoa wa Kivu Kaskazini. Ugonjwa huu huathiri zaidi watoto walio chini ya miaka mitano, katika muktadha wa vurugu, umaskini, watu kuhama makazi yao, na upatikanaji mdogo wa huduma za afya.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kati ya mwezi Aprili na Novemba 2025, zaidi ya wagonjwa 3,000 walitibiwa na shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) katika maeneo haya mawili. Maafisa wa afya na wafanyakazi wa kibinadamu wanatoa wito wa usaidizi wa haraka ili kutokomeza ugonjwa huo, kulingana na Radio OKAPI.

Katika maeneo ya afya ya Katoyi na Kirotshe (Masisi), wagonjwa 1,856 walipata matibabu kati ya mwezi Oktoba na katikati ya mwezi Novemba 2025, ikiwa ni pamoja na wagonjwa 756 yenye matatizo, kulingana na MSF. Wakati huo huo, katika eneo la afya la Binza (Rutshuru), timu za MSF zinaripoti kuwa zimewatibu wagonjwa wengine 1,195, ikiwa ni pamoja na wagonjwa 355 walio kuwa kati hali ya hatari, kati ya katikati ya mwezi Aprili na Novemba.

Watoto, hasa wale walio chini ya miaka mitano, ndio wanaoathirika zaidi. Utapiamlo wa mara kwa mara miongoni mwa watoto waliohamishwa au wale wanaoishi katika hali hatarishi huzidisha visa vya surua. Afisa wa afya anataja mambo mengine kadhaa yanayochangia kuenea kwa ugonjwa huu:

Uhaba wa chanjo; kutoweza kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba; rasilimali fedha za kutosha; na kutofikika katika baadhi ya maeneo kutokana na vurugu, na kufanya iwe vigumu kutoa chanjo na kuwafikia walengwa.

MSF inasema inaendelea kuwatibu wagonjwa, kulaza wagonjwa hospitalini, na kuunga mkono kampeni za chanjo. Hata hivyo, mahitaji yanabaki kuwa muhimu sana, shirika hili la kibinadamu linasema. Mwezi Juni mwaka huu, karibu watoto 100,000 walio chini ya umri wa miaka mitano walichanjwa katika eneo la Masisi, kulingana an Radio OKAPI.

MSF inaripoti kuunga mkono kampeni mpya zilizopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Novemba/mapema mwezi Desemba huko Katoyi na Kirotshe, ikilenga makumi ya maelfu ya watoto wengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *