
Mahakama ya Urusi imewahukumu watu wanane kifungo cha maisha jela leo Alhamisi, Novemba 27, kwa kuhusika kwao katika mlipuko mkubwa ulioharibu kwa kiasi daraja maarufu linalounganisha Urusi na Rasi ya Crimea, iliyounganishwa mwaka wa 2014.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kufuatia kikao cha mahakama huko Rostov-on-Don (kusini mwa Urusi), wanaume hao wanane wote wamepatikana na hatia ya kuwa sehemu ya “kikundi cha wahalifu kilichopangwa” kilicholenga “kutekeleza shambulio” kwenye Daraja la Crimea, ambalo liliwaua watu watano mnamo mwezi Oktoba 2022, mahakama ya kijeshi ya kikanda imesema katika taarifa.
Mlipuko huo, ambao ulitokea miezi minane baada ya kuanza kwa mashambulizi makubwa ya Urusi nchini Ukraine, baadaye Kyiv ilidai kuhusika.
Alama ya kuunganishwa kwa Crimea
Daraja hilo lenye urefu wa kilomita 19, lililozinduliwa mwaka wa 2018 na Rais wa Urusi Vladimir Putin, kwa serikali ya Urusi, ni mojawapo ya alama za kuunganishwa kwa rasi ya Crimea ya Ukraine mwaka wa 2014. Sehemu kadhaa za daraja hili la barabara na reli, ambazo zimerekebishwa tangu wakati huo, zilianguka kwa kiasi mnamo Oktoba 8, 2022, wakati lori lililokuwa limejaa vilipuzi lilipolipuka kwenye moja ya njia.
Mlipuko huo mkubwa ulisababisha moto mkubwa kwa magari manane ya mafuta ya petroli na kuharibu sehemu mbili za daraja. Shambulio hilo liliwaua watu watano, akiwemo dereva wa lori, ambaye vilipuzi vyake vilikuwa vimepakiwa bila yeye kujua, kulingana na taarifa ya mahakama.
Wanaume hao wanane, ambao walikana hatia, wamekuwawakisikilizwa katika vikao vya faragha tangu mwezi Februari. Shambulio lingine, ambalo pia lilidaiwa na Kyiv, liliharibu daraja hilo kwa kutumia ndege zisizo na rubani mnamo mwezi Julai 2023. Tangu wakati huo, mamlaka ya Urusi imeongeza kwa kiasi kikubwa ufuatiliaji wa daraja hili, jambo ambalo linaruhusu kutumwa kwa wanajeshi na vifaa vya kijeshi katika Crimea iliyounganishwa.