Watu 44 wamepoteza maisha jijini Hong Kong huku wengine zaidi ya mia mbili wakiwa hawajulikani walipo,kufuatia mkasa wa moto ulioteketeza jumba lenye orofa 31.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mapema Alhamisi wazima moto bado walikuwa wakipambana kuzima moto huo na shughuli za kuokoa watu katika eneo hilo lenye makazi elfu mbili.
Jumba hilo lilojengwa kwa mti aina ya Bamboo lilishika moto wakati marekebisho yalipokuwa yakiendelea na madirisha yote yalikuwa yamefungwa hivyo watu wengu hawakufahamu haraka kuwa kuna moto.

Miongoni mwa watu waliofariki ni mmoja wa zima moto ambaye alipata majeraha makubwa ya kuungua usoni baada ya kupoteza mawasiliano na wenzake.
Msemaji wa serikali eneo hilo amesema watu 56 wametibiwa hospitalini na kuruhusiwa kuondoka huku wengine 16 wakiwa kwenye hali mahututi.

Polisi asubuhi hii wamesema wamewakamata watu watatu wanaoshukiwa kuhusika na kisa hicho baada ya kuacha vifaa vya kushika moto haraka kwenye eneo hilo wakati wa shughuli za ufundi ,hali inayosemekana kuwa chanzo cha moto huo.