Kauli hiyo imekuja wakati dunia inaendelea na kampeni ya siku16 za kuhamasisha umma kutokomeza ukatili wa kijinsia. Kaulimbiu ya kampeni ya mwaka huu ni, ukatili dhidi ya wanawake mtandaoni.”

Bi. Jeptoo amesema yeye na wanaharakati wenzake waliona si vyema mtu ambaye ni mdogo sana kama Agnes kupoteza maisha yake kupitia dhuluma za kijinsia, akiongeza kuwa mambo ya ukatili wa kijinsia yametoka mbali sana kuanzia enzi za mababu zetu.

“Wakati tulipoona inafikia mwenzetu kama Agnes ambaye alikuwa umri wa miaka 25 pekee anauawa, tukaona ni vema twende pale kwa jamii zetu tuzungumze na vijana wetu, wanaume, na wasichana wetu kuwa ukatili wa kijinsia si kitendo kizuri, kuna njia ambazo tunaweza kuzungumzia ili tusipigane.” Amesema Viola.

Mwanariadha wa Kenya na mwanaharakati wa wanawake na wasichana, Viola Jeptoo Lagat, ambaye pia ni mwanzilishi wa shirika lisilo la kiserikali la Tirop Angels akiwa katika picha ya pamoja na wanariadha chipukizi wanaokuja.

Mwanariadha wa Kenya na mwanaharakati wa wanawake na wasichana, Viola Jeptoo Lagat, ambaye pia ni mwanzilishi wa shirika lisilo la kiserikali la Tirop Angels akiwa katika picha ya pamoja na wanariadha chipukizi wanaokuja.

Je, ni hatua gani Kenya imechukua katika kutomeza ukatili wa kijinsia?

Viola anasema Rais wa Jamhuri ya Kenya alianzisha kamati ili kukabiliana na changamoto za dhuluma za kijinsia, kwa sababu Rais ameona dhuluma ya kijinsia ni kitu kikubwa sana ambacho kimetuathiri sisi Wakenya na sana sana wanawake. “Dhulma za kijinsia haziathiri tu familia au mtu binafsi. zinaathiri hadi taifa nzima.” Amesema Bi Jeptoo.

Ameongeza kuwa kamati hizo zinasaidia kuelimisha watu katika jamii kuhusu namna unavyoweza kujitetea wakati unakumbana na changamoto za ukatili wa kijinsia.

Haki za wanawake za kusikilizwa mahakamani.

Bi. Viola amesema kuwa nchini Kenya kumekuwa na uwakilishi wa wanawake katika kesi za mahakamani, ikiwa ni Pamoja na wanawake viongozi.

Hivyo anasema “sisi kama wanawake tumeona tofauti kidogo kwa sababu tuko na mtetezi wetu huko juu na tumeona pia yeye amekuwa akienda kotini kutetea wanawake. Anahakikisha kuwa anapigania wale wanawake ambao wamedhulumiwa na kuwahimiza wanawake waongee ili wapate kusaidika.

Pia amesema mtetezi huyo anaendeleza mafunzo kwa wanawake ili wajue haki zao, na hivyo “wakati unapodhulumiwa, unajua sheria inakulinda na unaweza kusaidika vipi.”

Ujumbe kwa wanawake na wasichana wanaopitia ukatili wa kijamii

“Wanawake tusione aibu, tuongee tunapopitia dhulma za kijamii kwa sababu tukinyamaza tunaumia na wengine watazidi kudhulumiwa.” Amesema Viola Jeptoo akiongeza kuwa, hakuna mtu atakayejua unapitia jambo fulani na hautaweza kusaidika usipoongea.” Kitu cha muhimu ni kuripoti unapodhulumiwa.

Bi. Viola anashauri waathirika wa ukatili wa kijinsia kuripoti kesi zao kwa polisi Ili wahusika waajibike na sheria ifuatwe. Anasema kkwa wanawake ambao wanasema “nimeenda polisi mara moja au mbili tatu na mhusika amekuja kuachiliwa na anaendelea kunidhulumu”, anasema msife moyo, endelea kuripoti na siku moja atachukuliwa hatua.

Wanawake tusione aibu, tuongee tunapopitia dhulma za kijamii kwa sababu tukinyamaza tunaumia na wengine watazidi kudhulumiwa.

Amewasihi waathirika pia kuzungumza na mashirika ya kiraia, kama Tirop Angels na bila shaka watasikilizwa na watasaidiwa.

Ametaja kuwa kupitia baadhi ya kina mama na wasichana wamepatiwa huduma za afya na fedha za hospitali kupitia shirika lake, na huduma za hifadhi kwa maeneo salama, na kama “unahitaji wakili tunakulipia wakili ili kesi yako iweze kusikilizwa.” Amesema Viola akiongeza kuwa kwa watoto ambao pia wamebakwa, wamehakikisha wanapata huduma muhimu za matibabu na kwa kushirikiana na mashirika mengine kama shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women, wameweza kuwapeleka katika maeneo salama na kuhakikisha wamepata haki zao za elimu.

Mwanariadha na mwanaharakati wa wanawake na wasichana kutoka nchini Kenya, Viola Jeptoo Lagat (kulia) ambaye pia ni Mwanzilishi wa shirika lisilo la kiserikali la Tirop Angels, akiendesha shughuli za kushikamana na wanawake nchini humo.

Mwanariadha na mwanaharakati wa wanawake na wasichana kutoka nchini Kenya, Viola Jeptoo Lagat (kulia) ambaye pia ni Mwanzilishi wa shirika lisilo la kiserikali la Tirop Angels, akiendesha shughuli za kushikamana na wanawake nchini humo.

Dhulma za mtandaoni

Hakuna kitu chochote kinachohalalisha mtu yeyote apigwe, auawe, au kunyang’anywa mali yake.

Bi. Viola anasema “wanawake tusimame na wanawake wenzetu” akitaja maoni ya kukandamiza wanawake, ambayo ameweza kufuatilia mitandaoni, mfano wengine wakisema mliona vile alivyokuwa akimuongelesha mume wake, ndio imesababisha kudhulumiwa.Hakuna kitu kinachohalalisha mtu yeyote achapwe au auawe, au kuchukuliwa mali yako. Kama watu hawawezi kukaa katika ndoa au uhusiano vizuri, ni bora kuachana ili tusifike mahali tunaumizana au kuuana.” Amesema Bi. Viola.

Kwa wanaume

Bi Viola amewasihi wanaume kusimama na wanawake akisema kuwa “hakuna taifa ambalo iltaendelea bila mwanamke na mwanamume.” Akiwakumbusha kuwa mwanamke anayedhulumiwa anaweza kuwa ni dada yenu, sisi ni watoto wenu, msije kuwa wale ambao mnachangia wanawake kuuawa ama kudhulumiwa, Si vema, ni jambo baya sana. “Lazima tukae kama kitu kimoja ili tuendelee kimaisha, kifamilia na pia kiuchumi.” Amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *