Marais wa DRC Felix Tshisekedi na wa Rwanda Paul Kagame wanatarajia kukutana leo Alhamisi mjini Washington, nchini Marekani chini ya upatanisi wa Rais wa Marekani Donald Trump. Kuna uwezekano marais hao wawili kutia saini makubaliano ya amani, ikiwa ni miezi kadhaa kupita tangu makubaliano ya awali yaliyosimamiwa na Washington kushindwa kuzuia machafuko mwashariki mwa Congo.

Matangazo ya kibiashara

Marais wa DRC na Rwanda, Félix Tshisekedi na Paul Kagame, wanajiandaa kuidhinisha hati mbili ambazo tayari zimesainiwa na wawakilishi wao: makubaliano ya amani ya Juni 27 na mfumo wa ujumuishaji wa uchumi wa kikanda wa Novemba 7. 

Marais hao watakutana mjini Washington siku ya Alhamisi, Desemba 4. Mkutano huu, uliopangwa na Marekani, unakuja huku kukiwa na hali ya kutoaminiana kati ya wakuu hao wawili wa nchi, huku hali ya usalama mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikiendelea kuwa tete. Viongozi wengine wa Afrika wamealikwa kuwa mashahidi na, kwa baadhi, kama wadau katika mfumo wa kikanda ujao.

Ili kuelewa umuhimu wa mkutano wa Washington, ni muhimu kutazama nyuma mlolongo wa kidiplomasia ulioanzishwa miezi minane iliyopita. Mnamo Aprili 25, 2025, Kinshasa na Kigali zilitia saini “tamko la kanuni,” hati ya msingi iliyoweka wigo wa mazungumzo, moyo wa makubaliano yajayo, na lengo kuu: kukomesha mgogoro wa mpakani ambao ulikuwa umechochea ukosefu wa utulivu katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini kwa miaka mingi. Tamko hili, lililotiwa saini mbele ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, lilifungua njia ya makubaliano ya kina zaidi.

Makubaliano haya yalitiwa saini Juni 27 baada ya majadiliano magumu mbele ya Donald Trump. Mawaziri hao wawili wa mambo ya nje kisha wakarasimisha kile kilichowasilishwa kama “makubaliano ya amani ya uhakika.” Hata hivyo, nakala hiyo ilirejelea mara moja sehemu ya pili, iliyoonekana kuwa muhimu: mfumo wa ujumuishaji wa kiuchumi wa kikanda, ulioundwa ili kuimarisha amani katika mantiki ya ushirikiano wa kiuchumi. Hati hii, ambayo inaelezea maeneo ya ushirikiano, miradi ya pamoja, na ratiba, haikusainiwa hadi Novemba 7.

Makubaliano ya Juni 27 yaliidhinishwa na Bunge la Rwanda. Makubaliano ya Novemba 7 pia yanazingatiwa kwa kiasi kikubwa. Huko Washington, mkazo hautakuwa tena katika kujadiliana upya, bali katika “kuanzisha” makubaliano yote kisiasa, chini ya uangalizi wa washirika wa kikanda na kimataifa. Makubaliano ya pande mbili kati ya Marekani na DRC, na pia kati ya Marekani na Rwanda, pia yatasainiwa baadaye ili kuunda kile ambacho wasaidizi wa rais wa zamani wa Marekani unakiita “Mikataba ya Washington.”

Mkutano chini ya mvutano mkali kati ya viongozi wawili ambao hawazungumzi

Mazingira yanayozunguka kuwasili kwa marais hao wawili mjini Washington pia yanaonyesha udhaifu wa hali hiyo. Paul Kagame anawasili akiwa ameambatana na Waziri wake wa Mambo ya Nje. Vile vile Félix Tshisekedi. Lakini wawili hao hawaaminiani kabisa na hawajazungumza kwa miezi kadhaa.

Mnamo mwezi Oktoba, katika jukwaa la Ulaya huko Brussels, walipiga picha moja ya pamoja, bila hata hivyo kuzungmza. Kigali ilikataa hadharani ofa ya Félix Tshisekedi ya maridhiano. “Fursa hiyo sasa imepita,” kimetangaza chanzo kilicho karibu na Paul Kagame. Rwanda iliishutumu Kinshasa kwa kushindwa kutekeleza mifumo ya amani iliyopo na kuonya kwamba Tshisekedi hapaswi kuchukua usaidizi wa washirika wa kikanda kama jambo la kawaida.

Wiki moja kabla ya mkutano wa Washington, Paul Kagame aliendelea kuwa na shaka kuhusu matokeo ya mchakato huo. Kulingana na rais hyo wa Rwanda, “bado tuko mbali ya kumaliza mzozo huu,” na Kigali ilirudia kwamba “tayari kumekuwa na makubaliano ambayo Kinshasa haijayaheshimu.”

Kwa upande wa Kongo, msimamo huo umebadilika hatu kwa hatua. Mnamo Novemba 11, kwenye RFI, Patrick Muyaya, Waziri wa Mawasiliano, alisema kwamba “Rais Tshisekedi hatokwenda Washington kabla wanajeshi wa Rwanda kuondoka katika ardhi ya DRC.” Mstari huu mwekundu haukuendelezwa kwa maneno hayo haswa, lakini Félix Tshisekedi aliimarisha usemi wake katika mwelekeo mwingine. Kwake, Rwanda haiwezi kuunganishwa kikamilifu katika mfumo wa uchumi wa kikanda hadi itakapowaondoa wanajeshi wake katika ardhi ya Kongo na hadi uaminifu utakaporejeshwa.

Mjini Belgrade, akiwahutubia raia wa Kongo walio nje ya nchi, Rais Tshisekedi alitumia muda mwingi, siku nne kabla ya mkutano wa Washington, akihalalisha kile anachokiita “maono yake ya kimkakati.” Alirudia kwamba ushirikiano wa kiuchumi wa kikanda haukuwa wazo jipya. Mapema mwaka wa 2019, ulikuwa moja ya nguzo za sera yake ya kigeni. Wakati huo, alielezea nia yake ya “kuendeleza pamoja” miradi ya kibiashara na kiuchumi na majirani wa DRC.

Lakini sasa anadai kwamba ushirikiano huu unaweza kujumuisha Rwanda chini ya sharti moja tu: kujiondoa kwake kabisa katika ardhi ya Kongo na kurejesha uaminifu. “Hauwezi kufanya biashara na mtu ambaye humwamini,” alibainisha. Na anatoa wito kwa wanadiaspora kutopotoshwa na “matangazo.” Mkataba upo, utasainiwa, lakini “yote haya yatatumika tu ikiwa amani itapatikana kweli”.

Mkataba upo, utasainiwa, lakini “yote haya yatahesabiwa tu ikiwa amani itapatikana kweli.”

Sherehe chini ya uangalizi wa kidiplomasia

Siku ya Alhamisi, marais hao wawili watapokelewa kando kwanza kila mmoja na Donald Trump, kabla ya sherehe ya pamoja. Viongozi kadhaa wa Afrika, walioalikwa kama mashahidi na wadhamini, watakuwepo. Kwa hivyo Washington inatarajia kupanua mzunguko wa “wadhamini wa kisiasa” wa mchakato uliodhoofishwa na ukosefu wa uaminifu kati ya miji mikuu miwili na hali ya kijeshi inayoendelea kuzorota.

Kwa nini makubaliano haya yanaweza kushindwa kuleta amani?

Mojawapo ya vikwazo vikubwa inajulikana sana: kutokuwepo kwa hatua za kulazimisha. Tangu mwezi Oktoba, utaratibu wa kusitisha mapigano wa Kinshasa-AFC/M23 umekuwepo kwenye karatasi, lakini mapigano yanaendelea. Mhusika moja kwa moja katika uhasama ameiambia RFI kwamba jambo zima ni kama “ulaghai wa kimataifa,” mchakato bila vikwazo au utekelezaji.

Azimio la Baraza la Usalama nambari 2773, lililopitishwa mwezi Februari 2025, tayari lilidai kuondolewa kwa wanajeshi. Halijawahi kutekelezwa. Kwa hivyo, ufanisi wa mikataba mipya utategemea kabisa utashi wa kisiasa wa pande hizo. Na hii haipo.

Nguzo ya pili ya mfumo: mazungumzo ya Doha

Huko Washington, mchakato mwingine sambamba lazima uzingatiwe: ule uliofanywa Qatar na kundi la waasi la  AFC/M23. Mkataba wa mfumo ulisainiwa mnamo Novemba 15, 2025, kati ya Kinshasa na kundi hili la waasi. Huu bado sio mkataba wa mwisho wa amani, lakini ni hatua ya kati. Hati hiyo inajumuisha itifaki mbili ambazo tayari zimeanzishwa: moja kuhusu utaratibu wa uthibitishaji wa kusitisha mapigano, nyingine kuhusu kubadilishana wafungwa. Itifaki zingine bado hazijajadiliwa. Hapa tena, nakala zipo, lakini utekelezaji wake hauna uhakika. Mapigano bado yanaendelea na hali inaendelea kuwa “mbaya”, kulingana na AFC/M23.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *