
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Amnesty limetoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi huru kuhusu mashambulio yaliyofanywa na wapiganaji wa RSF kwenye moja ya kambi kubwa ya wakimbizi huko kaskazini mwa jimbo la Darfur, mwanzoni mwa mwaka huu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Katika ripoti yake Amnesty International imesema Mwezi wa Aprili mwaka huu RSF ilivamia kambi ya Zamzam na kuuteka mji wa el-Fasher na ikitekeleza ukatili wa kibinadamu ikiwa ni pamoja na kunyonga raia,ubakaji,unyanyasaji wa kijinsia, na uharibifu wa shule, misikiti pamoja na hospitali.
Ripoti hiyo ya Amnesty ni mojawapo ya ripoti za hivi punde za mashirika ya kutetea haki za binadamu kuishtumu RSF kwa vitendo vya ukatili katika vita vya takariban miezi 30 vya Sudan, hasa eneo la Darfur wakati huu pia Jeshi la Sudan vile vile likishutumiwa kwa ukatili huohuo.
Makabiliano kati ya RSF na jeshi la Sudan yalizuka mwezi Aprili 2023, Mgogoro huu ukisababisha vifo vya watu karibia laki 4 na kuwaacha wengine millioni 14 bila makao.