Novemba 30, 2025 jiji la Dar es Salaam lilishuhudia ugeni mkubwa wa kampuni zenye ushawishi zaidi barani Afrika ambazo zilikusanyika kwa ajili ya usiku wa tuzo za chaguo la mtumiaji Afrika 2025 (Consumer Choice Awards Africa 2025).
Katika tukio hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam, Doweicare Technology Company Limited wazalishaji na wasambazaji wa bidhaa za softcare zinazoaminiwa na mamilioni ya watu barani Afrika iliibuka moja kati ya kampuni zilizofanya vizuri zaidi.
Hii ni baada ya kushinda tuzo za; Most Trusted Sanitary Pad Brand in Tanzania and Most Quality Baby Diaper Brand in Tanzania 2025 zinazoifanya kuendelea kuwa kampuni inayoongoza katika uzalishaji wa bidhaa za usafi za watoto na wanawake Afrika. Zikiwa miongoni mwa tuzo zinazoaminiwa zaidi na watumiaji Afrika, tuzo hizi zinatambua na kuzitunuku kampuni ambazo zinafanya vizuri katika uzalishaji wa bidhaa bora, zinazoaminiwa na wateja pamoja na kuongoza katika soko la Afrika.
Ushindi huu haukuja kwa bahati, bali ni matokeo ya uwekezaji mkubwa wa kampuni katika teknolojia ya uzalishaji, utafiti wa bidhaa na mfumo madhubuti wa kuhakikisha wateja wanapata kile wanachokihitaji kwa ubora wa juu.
Historia ya Doweicare: Kutoka biashara ndogo mpaka kampuni inayoaminika zaidi Tanzania
Historia ya biashara ya bidhaa za usafi za watoto na wanawake ya Doweicare inaanzia mwaka 2009, wakati mtangulizi wa Softcare (kampuni mama ya Doweicare) ilipozindua baby diapers za Softcare nchini Ghana, ikiashiria kuingia kwake katika soko la Afrika. Mwaka mmoja baadaye, kampuni hiyo ilianza kufanya biashara ya baby diapers na sanitary pads nchini Kenya na Tanzania chini ya chapa ya Clincleer na kuenea katika soko la Afrika Mashariki.
Bidhaa kuu za Softcare barani Afrika.
Baada ya zaidi ya miaka 15 ya maendeleo barani Afrika, Softcare sasa imekuwa kampuni inayoongoza katika sekta ya bidhaa za usafi za watoto na wanawake katika nchi mbalimbali barani Afrika. Kwa mujibu wa takwimu za Frost & Sullivan, mwaka 2024 Softcare ilishika nafasi ya kwanza katika soko la baby diapers na sanitary pads barani Afrika hii ni katika nyanja ya mauzo.
Kwa Tanzania, Doweicare inaongoza katika mauzo ya bidhaa za usafi za watoto na wanawake jambo linalotokana na uzalishaji wa ndani pamoja kufanya vizuri katika soko.
Mwaka 2023 na 2024, Doweicare ilipokea Cheti cha Ubora kutoka kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kutambua mchango wake katika kulipa kodi ndani ya miaka yote miwili ya fedha. Mwaka 2024, kampuni hiyo ilitunukiwa Tuzo za Consumer Choice Awards Africa 2024 Most Quality Sanitary Sanitary Pads Brand in Tanzania.
Aidha, mwaka 2025 kampuni hiyo imeendelea kupata mafanikio na kutambulika kitaifa na kimataifa kwa kufanikiwa kutwaa tuzo ya Best Brand Africa (Baby Diaper) 2025, Most Trusted Sanitary Pad Brand in Tanzania, na Most Quality Baby Diaper Brand in Tanzania 2025, zinazoonyesha kukubalika kwa kampuni hiyo na kukuwa kwake katika nyanja za kimataifa. Yafuatayo ni mambo muhimu nyuma ya mafanikio haya:
Dhamira ya Doweicare katika kukuza uchumi wa Tanzania
Bidhaa zote za Doweicare zinazalishwa hapa nchini hivyo kuifanya kuwa kampuni kinara katika kukuza uchumi wa nchi kupitia utoaji wa ajira na kujenga uwezo kwa wazawa. Kupitia hilo, hadi sasa, Doweicare imezalisha ajira za moja kwa moja kwa Watanzania takribani 1000 sawa na asilimia 95 ya wafanyakazi wote wa kampuni hiyo.
Zaidi ya hayo, Doweicare imepanga kikamilifu katika kuzalisha bidhaa bora, ikionyesha dhamira yake katika kuunga mkono na kukuza ajenda ya kitaifa ya maendeleo ya viwanda. Kama kampuni, wanashiriki kikamilifu katika kutekeleza sera za Serikali ya Tanzania kuhusu maendeleo ya viwanda vya ndani, kuchangia katika uzalishaji wa ajira, ukuaji wa uchumi, na kuimarisha dira ya ‘Proudly Made in Tanzania’.
Upatikanaji wa uhakika wa bidhaa
Kupitia uzalishaji endelevu wa bidhaa zake, Doweicare inahakikisha kuwa bidhaa zake zinapatikana sokoni kila wakati. Bidhaa za Doweicare zinapatikana kwa wingi kupitia maduka makubwa, maduka ya jumla na rejareja na majukwaa ya mtandaoni kote nchini. Hii imeongeza imani ya wateja, wakijua kwamba wakati wowote wakihitaji bidhaa za Doweicare, wanaweza kuzipata kwa wakati.
Ushirikiano kutoka kwa wateja wetu: Nguzo ya mafanikio
Nyuma ya mafanikio ya Doweicare ni ushirikiano mkubwa wanaoupata kutoka kwa wateja wake. Wateja wamekuwa na imani kubwa na bidhaa za kampuni hiyo kutokana na ubora pamoja na upatikanaji wake. Hii imesababisha Doweicare kuendelea kuaminika na kulitawala soko la bidhaa softcare.
Kwa sasa, Doweicare inaongoza soko la bidhaa za usafi. Uongozi wake katika soko umejikita katika ubunifu endelevu, uzalishaji wa bidhaa zenye ubora wa kimataifa na uaminifu mkubwa kutoka kwa wateja wake.
Uzinduzi wa bidhaa mpya
Hivi karibuni Doweicare Technology Company Limited imezindua bidhaa mbili mpya ambazo zimepokelewa vizuri sokoni. Bidhaa hizo ni; Cuettie baby dippers na Softcare Sanitary Pads (Green pads).
Cuettie baby dippers
Bidhaa hii imeundwa kwa teknolojia mpya inayozingatia ngozi za mtoto. Ina unyonyaji wa haraka, inapitisha hewa vizuri na imehakikishwa kutokuwa na kemikali hatarishi. Wazazi wengi wameziona kuwa salama, laini na zenye ubora wa kipekee.
Softcare Sanitary Pads (Green pads)
Hii ni pedi yenye harufu nzuri ya mchaichai iliyotengenezwa mahususi kwa ajili ya mwanamke wa kisasa anayehitaji amani, usafi na kujiamini wakati wote. Pedi hii ina ukubwa wa 350 mm kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya wateja yaliyokuwepo na zina ubora zaidi, upana zaidi, laini na ya kipekee
Tuzo ambazo kampuni ya Doweicare Technology Company Limited imeshinda kwenye Consumer Choice Awards Africa 2025.
Softcare Sanitary Pads imelenga watumiaji wanaojali usalama wa afya pamoja na uhifadhi wa mazingira. Uwepo wa teknolojia ya harufu safi ya mchaichai na unyonyaji wa kiwango cha juu umeifanya Green Pads kuwa chaguo lenye mvuto mkubwa sokoni.
Kupitia bidhaa hizi mbili, Doweicare imeendelea kuonyesha utofauti na ubunifu unaojibu mahitaji ya kizazi cha sasa na baadaye.
Mikakati ya Baadaye: Ujenzi wa kiwanda kipya na ubunifu zaidi
Kwa kuangalia mustakabali wa kampuni na mahitaji yanayoongezeka, Doweicare inaendelea kutekeleza mikakati mikubwa ikiwamo: Ujenzi wa kiwanda kipya ambao umemalizika mkoani Pwani, kitakachoongeza uwezo wa uzalishaji na kutoa ajira mpya kwa wananchi.
Kuendelea kuleta bidhaa mpya zenye viwango vya kimataifa, zinazotumia teknolojia rafiki kwa mazingira na salama kiafya, kuimarisha mfumo wa usambazaji ili kuhakikisha bidhaa zinapatikana maeneo yote kwa urahisi zaidi na kuendeleza ubunifu na utafiti ili kuendelea kuwa kinara katika soko la Afrika Mashariki na kupanua wigo barani Afrika.
Doweicare na mkakati wa kurudisha kwa jamii
Mbali na kuzalisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu, Doweicare imeweka msingi imara wa kusaidia jamii kupitia mkakati wake wa CSR.
Ndani ya mwaka 2025, kampuni hiyo imeendelea kuonyesha ni kwa namna gani inashirikiana na kuzisaidia jamii nchini. Mfano Juni mwaka huu kampuni hiyo ilitoa baby diapers kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, ikiwa ni sehemu ya dhamira yake endelevu ya kuimarisha afya na utu wa familia za Kitanzania. Msaada huo pia ulielekezwa kwenda katika halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma.
Kampuni hiyo pia ilitoa jumla ya paketi 110,000 za diapers kwa ajili ya kuwasaidia kinamama wote wanaojifungua kwenye hospitali za Mkoa wa Dodoma. Lengo la msaada huu ni kulinda afya za watoto wachanga na kupunguza mzigo wa gharama za kifedha kwa familia.
Ujumbe kwa wateja
Katika hafla ya upokeaji wa tuzo hizo, uongozi wa Doweicare ulitoa shukrani kwa wateja wake kwa kuendelea kuamini bidhaa zao. “Ushindi huu wa kimataifa ni wa Watanzania na watumiaji wote wa bidhaa zetu. Bila ninyi, Dowcare isingefika hapa. Tunawashukuru kwa kutuamini na kuwa sehemu ya safari yetu,”
Ushindi wa tuzo tatu za Consumer Choice Awards Africa 2025 ni ishara kwamba Doweicare Technology Company Limited si tu chapa ya biashara, bali ni taasisi inayoongoza kwa ubunifu, kujali mteja na kutoa bidhaa zinazobadili maisha ya watu. Wakati kampuni ikiendelea kupanuka na kuleta masuluhisho mapya sokoni, matarajio ya watumiaji ni kuona ikiendelea kuwa alama halisi ya ubora barani Afrika.
Ikiendelea kukuza shughuli zake za uzalishaji na kuingiza bidhaa mpya sokoni, Doweicare itaendelea kuwa chaguo sahihi kwa wateja wake. Kupitia uzalishaji wa ndani, kampuni hiyo inalenga kuzalisha ajira endelevu, kukuza maendeleo ya kiuchumi na zaidi ya yote, kuhakikisha kuwa bidhaa hizo muhimu za usafi wa mwili zinapatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu kwa familia za Kitanzania na barani Afrika kwa ujumla.