“Tunaishauri Serikali kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kupanga na kutekeleza shughuli zao kwa utaratibu utakao wawezesha Watanzania kutumia kikamilifu haki hizi za msingi.

Mami ya watu wameripotiwa kuuwawa na zaidi ya watu 2000 wamewekwa vizuizini na vyombo vya usalama baada ya kutokea kwa maandamano kufuatia uchaguzi mkuu wa taifa hilo uliofanyika tarehe 29 Oktoba 2025.

Serikali imezidisha msako dhidi ya wapinzani tangu kupigwa kura. Tarehe 3 Desemba, polisi walitoa tangazo la kupiga marufuku nchi nzima maandamano yote ya Siku ya Uhuru.  Tunatoa wito wa kuondolewa kwa tangazo hilo kwani ni hatua isiyo na uwiano.

Tunavikumbusha vikosi vya usalama lazima vijiepushe na kutumia nguvu kutawanya mikusanyiko isiyo na vurugu na kufanya kila juhudi ya kupunguza mivutano. Tunawakumbuka tena matakwa ya sheria ya kimataifa katika eneo hili– kama hayawezi kuepukika, matumizi yoyote ya nguvu, ikiwa ni pamoja na silaha zisizo hatari sana, lazima yazuiliwe kwa kiwango cha chini kinachohitajika. Silaha za moto hazipaswi kutumika kutawanya watu kama hatua ya mwisho ya kukabiliana na kifo na inaweza tu kuwa njia ya kukabiliana na hatari ya kifo au majeraha makubwa.. Makamanda wa vikosi vya usalama wana wajibu wa kuchukua hatua kabla ya maandamano yoyote kuhakikisha kanuni hzi zina heshimiwa.

Ripoti mbalimbali zinaonesha kuwa tangu katikati ya mwezi Novemba, makumi ya watu wakiwemo wasomi, watendaji wa asasi za kiraia na viongozi wa kisiasa wa eneo hilo wamewekwa vizuizini, huku kukamatwa kwa watu kadhaa kukidaiwa kufanywa na watu wasiojulikana.

Usambazaji wa maafisa usalama umeongezwa katika maeneo ya  mijini, maonyo yamekuwa yakitolewa kwa maeneo ya biashara, vikwazo vilivyowekwa kwa uuzaji wa mafuta, na ufuatiliaji wa mawasiliano ya kidijitali umeongezeka. Hatua kama hizo huhatarisha kuchochea mvutano wa umma na kudhoofisha kwa kiasi kikubwa haki za uhuru wa kujieleza, kukusanyika kwa amani, na kushiriki katika masuala ya umma.

Wiki tano baada ya uchaguzi, mamlaka bado hazijatoa taarifa kuhusu idadi ya watu waliouawa na mazingira ya vifo vyao, na ripoti za watu kutoweshwa kwa nguvu. Kuendelea kutokuwepo kwa taarifa za uwazi kunahatarisha zaidi kuondosha imani ya umma na kuongeza mvutano katika wakati muhimu.

Tunatoa wito wa kuachiliwa mara moja na bila masharti wale wote waliokamatwa kiholela.

Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa inafahamu kuhusu serikali kuanzisha uchunguzi  kuhusu ghasia za baada ya uchaguzi. Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk anakumbusha kuwa uchunguzi kama huo lazima ufuate viwango vya kimataifa vya uhuru, kutopendelea, ukamilifu, uharaka na uwazi, na ulinzi mkali dhidi ya kulipiza kisasi, vitisho, kizuizini kiholela kwa wale wote wanaojihusisha na kazi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *