Kwa kushirikiana na Mpango wa Kimataifa wa Kutokomeza Polio (GPEI) unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, vinara hao wamezindua kampeni ya tokomeza polio au ‘Kick Out Polio’  kabla ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025, litakaloanza kusakatwa nchini Morocco tarehe 21 Desemba.

“Polio ni ugonjwa ambao tunapaswa kuchukua kwa uzito mkubwa,” amesema Naby Keïta wa timu ya taifa ya Guinea ambaye anachezea klabu ya Ferencváros ya Hungary.

Mashujaa wengine wa soka katika kampeni hiyo ni Sébastien Haller  kutoka Côte d’Ivoire, Fabrice Ondoa  kutoka Cameroon, Rodolfo Bodipo Díaz kutoka Equatorial Guinea, Michael Essien kutoka Ghana, na Bruno Ecuele Manga kutoka nchini Gabon.

Maendeleo na changamoto

Miongo ya ushirikiano wa kimataifa imepunguza polio ugonjwa unaoambukiza sana na kuathiri mwili, uliokuwa ukilemaza zaidi ya watoto 1,000 kila siku kwa mujibu wa takiwmu za Shirika la Afrya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO.

Juhudi hizi zimeokoa takribani watoto milioni 20 dhidi ya kupooza mwili na maisha milioni 1.5, kwa mujibu wa GPEI.

Ushirikiano huo wa umma na binafsi unangozwa na serikali za kitaifa na washirika sita, likiwemo Shirika la Afya Duniani WHO na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF.

Hata Afrika ikijivunia maendeleo makubwa kuelekea kutokomeza polio, milipuko bado inaendelea katika baadhi ya nchi, ikiweka watoto hatarini.

WHO inasema maendeleo ya kutokomeza ugonjwa huu yanatishiwa na upungufu wa fedha, migogoro, hofu ya chanjo, na mifumo dhaifu ya afya, na kufanya hatua ya mwisho ya kutokomeza polio kuwa ngumu zaidi.

“Ndoto yangu ni kuona Afrika ikitokomeza kabisa polio. Afrika, ni zamu yetu kutoa kadi nyekundu kwa polio,” amesema Fabrice Ondoa, ambaye awali alikuwa akichezea timu ya taifa ya Cameroon.

Changamoto ya mitandao ya kijamii

Nyota hao wa soka wanaeleza safari zao za uvumilivu na wamezindua changamoto mitandaoni kuonesha wazazi na viongozi kuwa changamoto ngumu zinaweza kushughulikiwa.

Wakiwa kwenye “muda wa nyongeza wa mchezo dhidi ya polio, wanawaalika watu kuchukua vitu vinne mpira, chupa, simu, na rafiki.”

Lengo ni kupiga chupa kutoka umbali mrefu zaidi na kumtaja mtu anayepaswa kuchukua changamoto ya #KickOutPolio.

Baada ya hapo, piga picha au rekodi video, iwekwe mitandaoni, na tag rafiki pamoja na mchezaji wako wa soka unayempenda, ukitumia hashtag ya kampeni.

“Tunajua kwamba Afrika ina tatizo kubwa la polio na lazima tupambane dhidi ya ugonjwa huu hatari sana. Sasa ni zamu yako,” amesema Rodolfo Bodipo Díaz, ambaye awali alichezea timu ya taifa ya Equatorial Guinea na klabu ya Hispania Deportivo Alavés.

Mvulana mwenye umri wa miaka kumi anacheza soka katika kambi ya wakimbizi wa ndani huko Abushok, Sudan.

© UNICEF/Mustafa Abdalrasol

Mvulana mwenye umri wa miaka kumi anacheza soka katika kambi ya wakimbizi wa ndani huko Abushok, Sudan.

Ushirikiano wa kimataifa

Licha ya changamoto zinazoendelea, Afrika inaendelea kuchukua hatua kubwa kupambana na polio.

GPEI imebainisha kuwa nchi 15 zimewachanja karibu watoto milioni 200 dhidi ya polio kati ya Januari na Oktoba mwaka huu.

Ameongeza kuwa “Kampeni zilizoratibiwa kanda kwa kanda kutoka Pembe ya Afrika hadi Bonde la Ziwa Chad na Sahel zimeonesha nguvu ya ushirikiano wa kuvuka mipaka, zikilinda mamilioni ya watoto.”

Ushindi mkubwa unakuja

Kampeni ya Kick Out Polio inahimiza kila mtu barani Afrika kusaidia kuchanja kila mtoto ili ugonjwa huu utokomee kabisa.

“Nimekabiliana na changamoto nyingi katika taaluma yangu ya soka hadi kufikia hapa nilipo sasa. Kwa njia hiyo hiyo, ninaamini Afrika inaweza kushinda changamoto ya kutokomeza polio na kufanikisha mustakabali wa bila polio,” amesema Michael Essien, aliyewakilisha Ghana na klabu ya Chelsea FC.

Bruno Ecuele Manga amewataka viongozi wa Afrika kusimama pamoja dhidi ya polio, akisisitiza kuwa Tunahitaji kuishinda polio kwa sababu tunahitaji vijana wa Afrika, ambao ndio mustakabali wa bara hili”.

Sébastien Haller ameongeza kuwa “Afrika, polio ni tatizo kubwa la kiafya, hasa kwa watoto. Wakati polio itakapokuwa historia, itakuwa ushindi mkubwa.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *