Dar es Salaam. Moja ya sifa kubwa ya wasanii wa jana, ni ubunifu. Walitumia akili sana kutengeneza wimbo au vesi. Mmojawapo ni Mb Dog, ambaye aligeuza majina ya vituo vya radio kuwa vesi kamili katika dude lake la Dear. 

Kuna Mapenzi Yanarun Dunia wa Alikiba. Wengi hudhani anaimbia dem, ukweli anamuimbia msela ambaye alisababisha dem wake ajiue. Kwa kumtuhumu kutoka na Kiba, wakati siyo kweli walikuwa washikaji. 

Hapa nakupa vesi ya Mb Dog katika pini lake la Dear. Anasema hivi: Huamini miujiza mchumba,

Sauti ya ‘nyuki’ inasikika… (Nyuki Dj wa Clouds Fm). Hili lilikuwa kundi la madj kadhaa wa Clouds, waliounda umoja na kujiita Nyuki Djs.

Sogea karibu ‘baby’ ‘time’ zishafika… (Times Fm).
Unipe ‘uhuru’ ‘dear, ‘nikiss’ nnapotoka… (Uhuru Fm, Kiss Fm kaunganisha).
Tukae mlimani dear, niwe ‘free’ ndani ya kopa… (Radio Mlimani na Radio Free Afrika).

Penzi kwa fujo my boo, moyo wangu ushauteka… (Kwa Fujo Djs). Kama Nyuki Djs, hili ni kundi la madj kadhaa wa vituo viwili vya radio, Radio One na Magic Fm, lililoongozwa na Aboubakar Sadiq na Dj Majay (Majizzo).

Hawa Kwa Fujo Dj, kwa kiasi kikubwa, walichangia ujio wa Raha P, rapa wa kike ambaye baadaye aliondoka Bongo. Na pia wakawa kimbilio la wasanii wengi wachanga
Raha ya Afrika RTD, mimi ndo ‘one naskika… (RTD ni TBC na One ni Radio One).

Hivi kwanini dear, moyo wangu unautesa… Hivi hushoboki dear, inavyonipenda East Africa…. (East Africa Fm).

Yii yii dear… 
I need you dear Ooh dear, I Love you my baby
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *