
Wanafunzi mia moja kutoka shule ya kikatoliki magharibi mwa Nigeria, waliotekwa nyara mnamo Novemba 21 na watu wasiojulikana wenye silaha, wameachiliwa, chanzo cha Umoja wa Mataifa na ofisi ya rais wa Nigeria wametangaza siku ya Jumapili, Desemba 7, bila kutaja hali halisi ya kuachiliwa kwao.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wanafunzi kutoka shule ya kikatoliki ya St. Mary huko Papiri, Jimbo la Niger, watakabidhiwa kwa maafisa wa serikali katika eneo hilo Jumatatu, chanzo cha Umoja wa Mataifa kimesema. Kuachiliwa kwa wanafunzi hawa 100 kulithibitishwa kwa shirika la habari la AFP na msemaji wa ofisi ya rais wa Nigeria, Sunday Dare.
Wanafunzi walioachiliwa kutoka shule ya kikatoliki ya St. Mary huko Papiri, katika Jimbo la Niger, “watakabidhiwa siku ya Jumatatu”, chanzo cha Umoja wa Mataifa kimesema, kikibainisha kuwa wanafunzi hao wamewasili Abuja.
Kwa jumla, wanafunzi 303 na walimu 12 walichukuliwa kwa nguvu kutoka shule ya bweni ya St. Mary, moja ya matukio makubwa zaidi ya utekaji nyara nchini Nigeria, nchi inayokumbwa mara kwa mara na matukio hayo. Karibu hamsini kati yao waliweza kuwatoroka watekaji wao muda mfupi baadaye. Hakuna taaarifa za takriban watu 165 ambao bado wanafikiriwa kushikiliwa mateka.
“Tuliomba na kusubiri warudi; ikiwa ni kweli, basi ni habari za kutia moyo,” amesema Daniel Atori, msemaji wa Askofu Bulus Yohanna wa Dayosisi ya Kontagora, ambayo shule hiyo ni mali yake. “Hata hivyo, hatujaarifiwa rasmi na hatujapokea taarifa yoyote kutoka kwa serikali ya shirikisho,” ameongeza.
Wimbi kubwa la utekaji nyara nchini Nigeria mnamo mwezi Novemba
Utekaji nyara wa watu wengi ni hutokea mara kwa mara nchini Nigeria, mengi ya matukio hayo yakifanywa na magenge ya wahalifu, wanaojulikana kama “majambazi,” wanaotafuta fidia.
Wanafunzi 303 na walimu 12 walitekwa nyara mnamo Novemba 21 katika shule ya kikatolika ya St. Mary huko magharibi mwa Nigeria. Hakuna taarifa yoyote kuhusu watu 165 ambao bado wanafikiriwa kuwa mateka. Hili ni tukio kubwa la utekaji nyara katik historia ya Nigeria, nchi inayokumbwa mara kwa mara na matukio hayo.