Kamati imesem Mashambulizi haswa dhidi ya jamii za Fur, Masalit na Zaghawa, yanadaiwa kufanywa na Kikosi cha Msaada wa Haraka RSF na makundi washirika katika maeneo ya El Fasher, Darfur Kaskazini.

Sudan yakabiliwa na janga la watu kufurushwa

Katika uamuzi wake wa dharura chini ya taratibu za tahadhari za mapema, Kamati imeeleza kuwa hali ya kibinadamu nchini Sudan inazidi kuzorota.

Kwa sasa nchi ina watu milioni 7.2 waliofurushwa toka kwenye makazi yao nchini humo na zaidi ya wakimbizi milioni 3 katika mataifa jirani, idadi inayoathiriwa zaidi na baa la njaa na kuporomoka kwa upatikanaji wa huduma muhimu za kibinadamu.

Ukatili umefurutu ada baada ya kuanguka kwa El Fasher

Kwa mujibu wa Kamati kuanguka kwa El Fasher chini ya udhibiti wa RSF mnamo 26 Oktoba 2025, baada ya mzingiro wa zaidi ya siku 540, kumeambatana na ripoti za ukatili mkali. Kamati ilieleza hofu kubwa kuhusu taarifa za:

  • Mauaji ya kikabila
  • Kuteswa na kuuawa bila kufikishwa mahakamani
  • Kuwakamata raia kiholela
  • Kubakwa na ukatili wa kingono kutumika kama silaha ya vita
  • Mashambulizi dhidi ya vituo vya afya, ikiwa ni pamoja na kuua wagonjwa
  • Kunyimwa huduma za afya
  • Mashambulizi dhidi ya wahudumu wa misaada na kuzuiwa kwa usaidizi

Vurugu zaidi zakithiri Kordofan

CERD pia imeonesha wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa ukatili katika ukanda wa Kordofan, ambako mapigano kati ya Jeshi la Sudan SAF na RSF pamoja na washirika wao yanaendelea.

Kamati imezitaka mamlaka za Sudan kuchukua hatua madhubuti na za haraka kukomesha kuongezeka kwa vurugu za kikabila, uchochezi wa chuki na matumizi ya lugha ya kibaguzi na kudhalilisha.

Pia imetaka kufanywa kwa uchunguzi wa haraka, wa kina, huru na wa wazi kuhusu tuhuma za ukiukaji wa haki za binadamu na sheria za kimataifa za kibinadamu.

Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa wahusika wakiwemo walioko katika nafasi za uongozi wanapaswa kuwajibishwa na waathirika lazima wapatiwe fidia kamili, bila kujali kabila la mwathirika au mkosaji.

Ushirikiano na wapelelezi wa kimataifa ni muhimu

CERD imeitaka Sudan kushirikiana kikamilifu na Tume Huru ya Kimataifa ya Uchunguzi Kuhusu Sudan, hususan katika uchunguzi wa ukatili uliofanywa ndani na nje ya El Fasher.

Kamati imerejea wito wake kwa pande zote kusitisha mapigano mara moja, kuweka msingi wa kusitisha mapigano bila masharti na kuanza mazungumzo jumuishi yanayohusisha makundi mbalimbali ya kikabila nchini Sudan.

Hatua hizi, imesisitiza, ni muhimu kurejesha serikali inayoongozwa na raia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *