#HABARI: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, ametoa pongezi kwa Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama kwa kuhakikisha hali ya amani na utulivu nchini, hasa baada ya kuibuka fununu za uwepo wa maandamano yasiyo na kikomo.

Waziri Simbachawene ametoa kauli hii alipotembelea na kuzungumza na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), pamoja na Jeshi la Polisi katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, ambako vikosi hivyo vimekuwa vikifanya doria na kuimarisha ulinzi.

Waziri Simbachawene ameahidi kuwa Serikali itaendelea kuimarisha ushirikiano na vyombo vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kufanya shughuli zao bila wasiwasi, huku akisisitiza kuwa amani ni msingi muhimu wa maendeleo ya taifa.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *