Wajumbe kadhaa wa serikali ya mpito ya Mali wakiongozwa na Waziri Mkuu Abdoulaye Maïga wamefanya ziara ya kiserikali nchini Guinea siku ya Jumanne, Desemba 9, 2025. Mamlaka ya Mali inayokabiliwa na mashambulizi ya wanajihadi wa JNIM dhidi ya malori ya mafuta, inatafuta msaada kutoka Conakry. Masuala ya kimkakati yamlitawala majadiliano yao.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Conakry, Tangi Bihan

Ziara ya wajumbe wa serikali ya mpito ya Mali huko Conakry, Guinea, Jumanne, Desemba 9, 2025, ni sehemu ya ushirikiano wa siri kati ya nchi hizo mbili katika mapambano dhidi ya makundi ya wanajihadi. Pia inafuatia makubaliano ya pande mbili yaliyosainiwa Conakry mwezi Agosti mwaka huu kuhusu usafiri, usalama wa mipakani, na ufugaji wa mifugo. Haya yote ni masuala muhimu kwa nchi hizi mbili, ambazo zinashiriki zaidi ya kilomita 800 za mpaka.

Huenda ni shinikizo lililoongezeka kutoka kwa wanajihadi waliozunguka Bamako lililomfanya rais wa mpito wa Mali, Assimi Goita, kutuma ujumbe huu mwingine, wakiwemo mawaziri wa Ulinzi, Uchumi, Uchukuzi, na Mifugo, kwenda Conakry.

Waziri Mkuu wa Guinea anasema “anajali” utulivu wa Mali

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri Mkuu wa serikali ya mpito ya Mali, Abdoulaye Maïga, amesema “ameridhishwa sana” na mazungumzo yake na serikali ya Guinea, huku mwenzake wa Guinea, Bah Oury, akisema kwamba “anajali” utulivu wa Mali, ambao utulivu wa Guinea unategemea. Lakini hakuna waziri mkuu aliyekuwa tayari kufafanua jinsi Guinea inavyounga mkono Mali katika mapambano yake dhidi ya wanajihadi wa JNIM na kizuizi cha mafuta wanachojaribu kuweka Bamako.

Abdoulaye Maïga amesema haraka kwamba Guinea tayari ilikuwa imeisaidia Mali kukabiliana na vikwazo miaka mitatu iliyopita: wakati huo, ilikuwa ikiongozwa na ECOWAS, ambayo ilikuwa ikidai kuondoka  jeshi la Mali liondoke madarakani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *