Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), siku ya Jumanne, Desemba 9, 2025, imemhukumu kiongozi wa wanamgambo wa Janjaweed nchini Sudan Ali Kushayb kifungo cha miaka 20 jela, kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Uhalifu huu ulifanywa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka ishirini iliyopita katika jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan. Ni mbabe wa kwanza wa kivita wa Sudan kuhukumiwa na ICC.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Pamoja na mwandishi wetu huko Hague, Stéphanie Maupas

Ali Mohamed Ali Abd-Al-Rahman, anayejulikana pia kwa jina lake la kivita Ali Kushayb, alipatikana na hatia mnamo mwezi Oktoba 2025 kwa makosa mengi dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita, ikiwa ni pamoja na ubakaji, mauaji, na mateso yaliyofanywa kati ya mwaka 2003 na 2004 katika jimbo la Darfur, magharibi mwa Sudan.

Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu aliomba kifungo cha maisha jela: majaji wa ICC walitangaza siku ya Jumanne, Desemba 9, 2025, kifungo cha miaka 20 jela. Kutoka kwa hukumu hii, miaka mitano ambayo tayari ametumikia kizuizini kabla ya kesi tangu kujisalimisha kwake kwa Mahakama mnamo mwezi Juni 2020 ipunguzwa kwa miaka hiyo 20 aliyohukumiwa.

Mwanzo wa kutambuliwa kwa waathiriwa wa Darfur

Waathiriwa walikuwa wamewaachia majaji uamuzi wa hukumu lakini waliomba kwamba mtu huyo aliyehukumiwa asirudi Darfur. Kamanda wa zamani wa Janjaweed atakuwa na umri wa miaka 87 atakapoachiliwa kutoka gerezani. Jaji mkuu wa mahakama ya mwanzo, Joanna Korner, amesema kwamba kuhukumiwa pia ni kukiri uhalifu huo.

“Kuhukumiwa kwa Abd-Al-Rahman ni kutambuliwa kwa mara ya kwanza kwamba watu wa Darfur hawakuwa waathiriwa wa mgogoro rahisi wa kikabila, au kitu kama hicho. Walikuwa waathiriwa wa kampeni ya makusudi—mahakaam iiliweka wazi hili—iliyoongozwa na wale walio madarakani, iliyofanywa na Janjaweed, wakiongozwa na Bw. Abd-Al-Rahman katika eneo la Wadi Saleh, na chini ya mamlaka ya serikali ya Sudan,” jaji Joanna Korner alielezea.

Kwa waathiriwa wa Darfur, hukumu hii pia inaashiria mwanzo kabisa wa mchakato wa fidia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *