Licha ya wito wa maandamano dhidi ya Rais Samia Suluhu Hassan, hali ya utulivu iliendelea kuwa shwari katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania siku ya Jumanne, Desemba 9, 2025. Mwishoni mwa mwezi Oktoba, waandamanaji walidai rais ajiuzulu, na kusababisha ukandamizaji mkali kote nchini. Vitisho vilivyotolewa na rais na serikali yake katika siku za hivi karibuni vinaonekana kuzuia uasi wowote na kushinda hamu kubwa ya mabadiliko miongoni mwa vijana wa Kitanzania.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu jijini Dar es Salaam, Élodie Goulesque

Kwenye mitandao ya kijamii, siku ya Jumanne, Desemba 9, 2025, vyombo vingi vya habari vya Tanzania vilionyesha picha za miji iliyosalia tupu. Kwa kuzingatia hali ya jumla ya nchi, mji mkuu wa kiuchumi wa Tanzania, Dar es Salaam, pia hakuan mtu aliyejitokeza kuingia mtaani kufuatia onyo la serikali na vikosi vya ulinzi na usalama. Hata hivyo, jiji hilo lilikuwa mojawapo ya maeneo muhimu ya maandamano ya kudai kuondoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan mwishoni mwa mwezi Oktoba.

Ikumbukwe kwamba katika siku za hivi karibuni, maonyo dhidi ya waandamanaji yamekuwa yakitolewa kila mara. “Tuko tayari,” mkuu wa nchi alitangaza kuhusu wito wa maandamano katika Siku hii ya Uhuru. Serikali yenye ujasiri ambayo inaonekana imefanikiwa kuwatisha watu, ambao walipendelea kubaki majumbani mwao. Hata kwa wale waliojaribu kutoka: hakuna usafiri wa umma uliokuwa ukifanya kazi, na kuzuia harakati zozote za waandamanaji. Vizuizi vingi pia viliwezesha vikosi vya usalama kukagua na kuchunguza ni nani anayejaribu kuondoka nyumbani kwake na kwa nini.

Ukandamizaji wa umwagaji damu uliotokea mwishoni mwa mwezi Oktoba, ambao ulisababisha vifo vya zaidi ya watu 1,600, kulingana na chama cha upinzani cha Chadema.

Huku nchi ikiwa imejiandaa kwa siku hii kwa zaidi ya mwezi mmoja, huku wito wa maandamano ukiendelea kurushwa kwenye mitandao ya kijamii, Desemba 9 haikuwa na athari iliyotarajiwa kwa waandamanaji. Serikali, kupitia wawakilishi mbalimbali katika ngazi ya kikanda,  imekaribisha utulivu ulioshuhudiwa nchini siku ya Jumanne.

Waandamanaji, wanaodai Rais Samia Suluhu Hassan aondoke na hali bora ya kiuchumi, hawaachi mapambano yao: maandamano mapya yamepangwa kufanyika Desemba 25.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *