
Katika ripoti yenye kichwa “zaidi ya hesabu – Ripoti kuhusu hali ya unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana nchini Sudan (2023-2025),” Mpango wa Kimkakati wa Wanawake katika Pembe ya Afrika (SIHA) unaelezea unyanyasaji wa kijinsia uliowapata wanawake wa Sudan tangu kuzuka kwa vita mnamo Aprili 15, 2023, kati ya jeshi na wanamgamb wa RSF.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu wa kikanda, Gaëlle Laleix
Vita nchini Sudan vimekuwa na athari kubwa, haswa kwa wanawake na wasichana. SIHA imechapisha ripoti kuhusu unyanyasaji unaofanywa dhidi ya wanawake katika muktadha wa mzozo kati ya jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF).
Mateso, ubakaji, utekaji nyara, ndoa za kulazimishwa: shirika hilo linalaani mfumo wa uchokozi unaofanya unyanyasaji dhidi ya wanawake kuwa silaha ya vita.
Shirika hilo limerekodi karibu visa 1,300 vya unyanyasaji dhidi ya wanawake tangu kuanza kwa vita nchini Sudan. Hili ni tone la baharini ikilinganishwa na hali halisi, shirika linakiri, likielezea ugumu wa kukusanya taarifa.
Robo tatu ya vitendo hivi vya vurugu ni ubakaji
Zaidi ya robo tatu ya vitendo hivi vya vurugu ni ubakaji, na 87% vinahusishwa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF). Waathiriwa wana umri wa kuanzia miaka 4 hadi zaidi ya 60. Ubakaji huu unawalenga wanawake kulingana na kabila lao, kazi, na jamii wanakotoka.
Watafiti wameanzisha mfumo wa unyanyasaji wa kijinsia unaofanywa na RSF. Kwanza, wakati wa utekaji wa eneo, wapiganaji huwapora na kuwabaka wanawake majumbani mwao. Kisha, baada ya kujiimarisha, RSF huwabaka katika maeneo ya umma kama vile barabarani, mara nyingi katika wakiwa kwa makundi. Hatimaye, wapiganaji hunyakua udhibiti wa wanawake. Hufungiwa majumbani mwao, huwekwa kwa wapiganaji, na wakati mwingine hulazimishwa kuolewa.
SIHA pia inalaani vurugu zilizofanywa na jeshi la Sudan, hasa baada ya kukamatwa tena kwa mji wa Khartoum, ambapo baadhi ya wanawake walishutumiwa kushirikiana na RSF.
Kulingana na shirika hilo, vurugu hizi zinatokana na utamaduni mrefu wa kutokujali uliotekelezwa wakati wa migogoro ya awali ya Sudan huko Darfur, Kordofan, na katika Milima ya Nuba.
Nchini Sudan, vita kati ya jeshi na wanamgambo vimewaua makumi ya maelfu ya watu katika kipindi cha miaka miwili na nusu iliyopita, kusaabisha wakazi milioni kumi na mbili kutoroka makazi yao, na kuharibu miundombinu ya nchi hii ya Afrika Mashariki.