Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameungana na viongozi wengine wa serikali kutoa salamu za pole kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama, akimtaja kama mmoja wa viongozi waliokuwa na uwajibikaji wa kiwango cha juu katika utumishi wa umma.

Dkt. Mwigulu ameongeza kuwa kifo cha Jenista kimemshtua kwa kiwango kikubwa, akieleza kuwa siku za hivi karibuni walikuwa pamoja wakitekeleza majukumu ya kikazi, na hakuonyesha dalili yoyote ya kulalamika kuhusu matatizo ya kiafya. Amesema taifa limempoteza mtu aliyejitoa kwa moyo wake wote katika kuitumikia nchi.

@jamesbunuma
#Cloudsdigitalupdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *