Luca Zidane ambaye ni mtoto wa nyota wa zamani wa Ufaransa na Real Madrid, Zinedine Zidane, ataichezea timu ya Taifa ya Algeria katika Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baadaye mwezi huu huko Morocco.

Luca anayecheza nafasi ya kipa, ameteuliwa kuwemo katika kikosi cha mwisho cha Algeria kitakachoshiriki Fainali hizo zitakazoanza Desemba 21.

Kabla ya hapo, Luca Zidane mwenye umri wa miaka 27 anayechezea timu ya Ligi Daraja la Kwanza Hispania, Granada, alidakia timu zote za taifa za vijana za Ufaransa.

Mechi yake ya kwanza kuichezea Algeria mara baada ya kuamua kutumikia timu hiyo ya taifa badala ya Ufaransa ilikuwa ni dhidi ya Uganda miezi miwili iliyopita ambao ulikuwa wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026.

Kikosi hicho cha Algeria kinaundwa na makipa: Luca Zidane (Granada), Oussama Benbot (USM Alger) na Anthony Mandrea (Caen)

Mabeki ni Rafik Belghali (Verona), Rayan Aït-Nouri (Manchester City), Youcef Atal (Al-Sadd), Mehdi Dorval (Bari), Jaouen Hadjam (Young Boys), Zinedine Belaid (JS Kabylie), Ramy Bensebaïni (Borussia Dortmund), Samir Chergui (Paris FC), Aïssa Mandi (Lille) na Mohamed Tougai (Esperance).

Viungo ni Ismael Bennacer (Dinamo Zagreb), Rami Zerrouki (Twente), Adam Zorgan (Union Saint-Gilloise), Hicham Boudaoui (Nice), Houssem Aouar (Al-Ittihad), Ibrahim Maza (Bayer Leverkusen) na Fares Chaibi (Eintracht Frankfurt)

Washambuliaji ni Mohamed Amoura (Wolfsburg), Ilan Kebbal (Paris FC), Riyad Mahrez (Al-Ahli), Anis Hadj Moussa (Feyenoord), Adil Boulbina (Al-Duhail), Monsef Bakrar (Dinamo Zagreb), Baghdad Bounedjah (Al-Shamal) na Redouane Barkane (Al-Wakrah).

Katika Fainali za AFCON 2025, Algeria imepangwa kundi E na timu za Guinea Ikweta, Burkina Faso na Sudan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *