Roz Saini anasema ana umri wa miaka 21, anauliza upweke, labda upo kwa kila mtu, sivyo? unakuwepo katika maisha ya watu wote, siyo?

Katika kipindi cha ukuaji wa Roz, maisha ya nyumbani kwao hayakuwa na utulivu, na hakupata msaada wowote kutoka kwa jamii iliyokuwa ikimzunguka.

“Nilikuwa darasa la sita nilipopata kujua kuhusu baba yangu. Niliporudi nyumbani kutoka shuleni, niliona umati wa watu mbele ya nyumba yetu. Nilikuwa mdogo sana wakati huo, na nikaona polisi walikuwepo.Nilihisi upweke mkubwa sana wakati baba yangu alipokuwa akirudi nyumbani akiwa amelewa. Ilikuwa vigumu sana kwangu kuona mambo hayo. Nilijua kuhusu matatizo tuliyokuwa tukikabiliana nayo, kwamba wangeweza kuamua kutupeleka kwenye nyumba ya watoto yatima, tukiwa peke yetu kabisa. Nilikuwa nikifikiria mambo haya yote… samahani.”

Roz, nini kilifuata baada ya hapo?

“Jamii ilijitenga na familia yetu. Hali hii iliendelea kwa muda fulani, na hatimaye tukafukuzwa kwenye nyumba tuliyokuwa tumepanga. Nilikuwa nimekaa nje barabarani pamoja na mali zetu za nyumbani, na wakati huo ndipo nilihisi upweke mkubwa kuliko wakati mwingine wowote maishani mwangu. Nilitamani sana kama kungekuwa na mtu yeyote karibu nami wakati huo, hata kama angekuwa ni baba yangu. Kama jamii ingekuwapo kwa ajili yetu na kutupa msaada, hata kidogo tu, basi huenda mama yangu asingehisi kukata tamaa kiasi kile. Niliacha kuzungumza na watu, nikaanza kutumia muda mwingi peke yangu. Upweke ukawa kama rafiki yangu, lakini pia ulinipa msukumo wa kujifanyia jambo. Jamii… jamii ina nafasi muhimu sana katika familia, sivyo?

Kwa Sasa unafanya nini Roz?

“ Hivi karibuni nimeanza kazi ya ustawi wa jamii. Sikuwa nimewahi kufikiria kuwa ningekuwa mfanyakazi wa ustawi wa jamii. Haikuwa rahisi kwangu; baada ya kumaliza kidato cha sita nilihisi kulikuwa na haja ya kusaidia familia yangu kifedha. Nilianza kuzungumza na watu katika jamii, nikaanza kushiriki nao.”

Nini kinafuata Roz

“ Ningependa kushiriki mambo kwa uwazi na wengine, lakini ninaona ni vigumu kufanya hivyo. Hata hivyo, nilianza kushiriki katika shughuli za kijamii. Kizazi changu kinakabiliwa na shinikizo kubwa la kuonekana kuwa na furaha, na inaweza kuwa vigumu kushiriki matatizo binafsi katika mazungumzo ya kawaida. Nilihisi kuwa uhusiano wangu na wengine unaimarika zaidi tunapojifunua na kufunguka.”

Kupitia ustahimilivu mkubwa alioupigia Roz, amefanikiwa kushinda hisia kali za upweke, lakini uzoefu huo ulimfundisha kuwa uhusiano wa kijamii na hisia ya kuwa sehemu ya jamii ni muhimu kwa ustawi binadamu yeyote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *